JESHI LA POLISI NCHINI LAKITHIRI UVUNJIFU WA HAKI ZA BINADAMU,SOMA HAPO KUJUA
Jeshi la Polisi likifanya utesaji kwa raia |
JESHI la Polisi nchini limetajwa kuwa kinara wa
ukiukwaji wa haki za Binadamu kwa raia,kutokana na kukithiri vitendo vyake
vya kutesa raia pindi inapowatia
hatiani.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hayo yamesemwa leo na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu
na Utawala bora ,Dkt.Kevin Mandopi wakati kuadhimisha siku ya Afrika ya kuzinduliwa kwa muongozo wa Luanda
kuhusu haki za watuhumiwa wa makosa ya Jinai,wanapokamatwa na kuzuiliwa
mahabusu kabla ya kushtakiwa,
Amesema kwa mujibu wa taarifa mbali mbali za tume
hiyo,pamoja na malalamiko yanayopokelewa na tume kutoka kwa wananchi dhidi ya
jeshi la polisi ni zaidi ya asilimia 60 ya malalamiko yanaelekwa kwa jeshi la
Polisi kwa kukiuka haki za binadamu.
Amesema licha sheria ya Jeshi la Polisi ya mwaka 2002
kifungu cha 27 (3) kuwapa mamlaka polisi kumkamata mtu yeyote iwapo kunasababu za sheria kufanya hivyo
lakini amedai jeshi limetumia sheria hiyo kufanya uvunjifu wa haki za Binadamu.
Dkt Mandopi ametaja uvunjifu huo wa haki za badamu
unaofanywa na jeshi la Polisi ni kupigwa kwa Raia pindi
wanapokamatwa,kutofikishwa Mahakamani kwa kubabikiziwa kesi,kunyimwa dhamana
kutofikishwa mahakamani kwa wakati yanahusu kupigwa,kuteswa pamoja na
kucheleweshwa kwa upelelezi.
Dkt Mandopi amesema mambo hayo ni kinyume na matakwa ya muongozo wa
Luanda,katiba,sheria za nchi,mikataba ya kikanda na kimataifa ya haki za
bindamu.
Hata hivyo,Dkt Mandopi amesema kutokana hali
hiyo Tume za Haki za Binadamu na utawala
Bora,Chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) pamoja na Jukwaa la Haki na usalama
wameliomba jeshi la Polisi na taasisi za serikali kusimamia utekelezaji wa
mchakato wa jina ikiwemo kuzingatia muungozo wa kimataifa ili kuliondoa taifa
kwenye kazia hiyo
Hakuna maoni
Chapisha Maoni