UTT-PID yakanusha taarifa za uongo zinazosambazwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii
Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu ‘’UTT Projects and Infrastructure Development Plc’’ (UTT-PID) ni Taasisi inayomilikiwa na Serikali ya Tanzania na kuendeshwa chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.
Menejimenti ya UTT-PID imesikitishwa na kitendo cha moja ya gazeti la kila wiki linalotoka hapa Tanzania katika matoleo yake mawili yaliyopita ya mwezi wa Machi 7 na Machi 14, mwaka huu kwa kuandika habari zisizo sahihi bila kupata maelezo ya Taasisi husika kinyume na maadili ya uandishi wa habari yanayovitaka vyombo vya habari kuzingatia usahihi, haki na usawa katika kutoa habari yoyote.
Tunapenda kuujulisha Umma wa Watanzania kuwa baada ya Taasisi kufuatilia chimbuko la taarifa zisizo sahihi zinazotolewa na baadae kuandikwa kwenye gazeti hilo ilitoa taarifa kwa vyombo vya dola ambavyo vinafanyia uchunguzi suala zima la tuhuma na nani anazisambaza tuhuma hizo ambazo kimsingi zina lengo la upotoshaji na kuichafua UTT-PID.
Aidha Menejimenti ya UTT-PID inawashauri waandishi wa habari na wahariri wa habari wajikite kwenye weledi, ukweli na maadili ya tasnia ya habari, wafanye utafiti wa kina na kutoa taarifa zilizo sahihi na kwa umakini, uhakika na kutokubali kamwe kutumiwa na watu au makundi ambayo yana agenda binafsi katika kufikisha ujumbe wenye matakwa yao.
Mwisho tunawasihi wadau wetu katika miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya usimamizi wa UTT-PID, wateja wetu pamoja na Umma kwa ujumla kuendelea kuwa na imani na Taasisi ya UTT-PID kwa kuwa habari hizo ni za uzushi na zenye lengo la kuichafua Taasisi.
Waweaza kutembelea UTT-PID kuifahamu zaidi kupitia tovuti yao: www.utt-pid.org
TAARIFA HII IMETOLEWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA UMMA UTT-PID
GOLDEN JUBILEE TOWER 12 FLOOR. OHIO STREET
DAR ES SALAAM
18 MACHI 2016
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa UTT-PID, Dk.Gration Kamugisha (katikati-mbele) akizungumza na wanahabari mapema leo Machi 18.2016 juu ya kanusho za taarifa za uongo zilizotolewa na moja ya Gazeti la kila wiki hapa nchini dhidi ya taasisi hiyo.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa UTT-PID, Dk.Gration Kamugisha(kulia) akisikiliza swali kwa makini kutoka kwa mwandishi wa habari (Hayupi pichani). Kushoto kwake ni Ofisa Mwandamizi wa UTT-PID, Bw.Liberatus Banzunaki wakati wa mkutano wao huo kwa waandishi wa vyombo vya habari mapema leo Machi 18.2016.Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa UTT-PID, Dk.Gration Kamugisha (kushoto) akitoa taarifa ya kukanusha kwa vyombooo vya habari dhidi ya tuhuma zilizoandikwa na moja ya Gazeti la kila wiki juu ya taasisi hiyo.Kulia kwake ni Mkuu wa Operesheni na miradi wa UTT-PID, Bw. Aleksandar Nikolic
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa UTT-PID, Dk.Gration Kamugisha akifafanua jambo wakati wa kutoa kanusho hilo dhidi ya tuhuma za uongo zilizoandikwa na moja ya gazeti la kila wiki hapa nchini pamoja na mitandao ya kijamii. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog.com).
Hakuna maoni
Chapisha Maoni