CUF YAZIDI LAANI UTESAJI WA POLISI ZANZIBAR YAIBUKA YAKANA TUHUMA ZA POLISI,SOMA HAPO KUJUA
Hamid Bobal, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CUF (JuviCUF) |
JUMUIYA ya Umoja
wa Vijana ya Chama cha Wananchi CUF Taifa (JUVICUF) imesikitishwa na kitendo
cha Jeshi la Polisi visiwani Zanzibar kuwashutumu baadhi ya wanachama wa CUF na
kuwahusisha na matukio ya ulipuaji wa mabomu, anaandika Regina Mkonde.
Akizungumza na waandishi wa Habari Hamidu
Bobali, Mwenyekiti wa JUVICUF katika ofisi za makao makuu ya CUF jijini Dar es
Salaam leo, amesema mazingira ya ulipuaji mabomu hayo yalikuwa yenye utata
ambapo yanaashiria kuwa utekelezaji wa ulipuaji mabomu hayo ulipangwa.
Bobali ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mchinga amedai kuwa
ulipuaji huo unafanywa na baadhi ya wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“CCM kwa kushirikiana na vyombo vya usalama imekuwa ikijaribu
kuficha ukweli kuhusiana na Zanzibar. Kumekuwa na ulipuaji mabomu unaoendelea
visiwani humo, ambapo ukichunguza utaona mabomu yanayolipuliwa ni ambayo
mwananchi wa kawaida hawezi kumiliki,” amesema.
“Hata siku moja sijawahi sikia kuna nyumba imelipuliwa ambayo
haikuwa na watu ndani yake, nyumba zote zilizodaiwa kulipuliwa na wanachama wa
CUF hakukuwa na watu ndani yake,” ameongeza Bobal
Bobali amehoji “Kama kweli wanaolipua mabomu hayo wangekuwa
walipuaji kweli, wanheleta madhara makubwa, lakini cha kushangaza mabomu
hayakuwadhuru watu.”
Bobali amesema kuwa, nyumba iliyolipuliwa maeneo ya Kisonge
visiwani Pemba hivi karibuni, haikuwa na watu ndani yake wakati bomu
lilipolipuliwa, pia amesema kwenye nyumba ya Kamishna wa Polisi ambayo
ililipuliwa hakukuwa na mtu wakati wa utekelezaji wa tukio hilo.
“Matukio hayo mawili yanadhihirisha kwamba mashambulizi
yalipangwa, na kwa sababu Pemba kuna wananchama wengi wa CUF wameona bora
wawatupie lawama ili mwisho wa siku wakichafue chama na kuwafanya wanachama
kuonekana waanzilishi wa machafuko,” amesema.
Amesema,
kinachoendelea Zanzibar ni utumiaji mbovu wa vyombo vya dola pamoja na Jeshi la
Polisi kuvaa vazi la ukada jambo linalopelekea kusahau majukumu yao ya
kuwalinda wananchi pasipo kuangalia itikadi zao za vyama.
“Tumeshuhudia
watu wakipigwa lakini polisi hawakuchukua hatua yeyote, pia tumemsikia na
kushuhudia mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Juma akiandika maneno yanayolenga
uchochezi lakini hadi leo anaachwa akitamba uraiani,” amesema.
Bobali amesema,
Sadifa aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook maneno yasemayo “Vijana wa CCM
tumechoka kuchokozwa na JUVICUF,” ambapo aliamuru vijana wa CCM kuwashughulikia
vijana wa CUF.
“Hivi karibuni
nilikutana na Sadifa, nikamhoji juu ya kauli aliyoiandika ili nijue kama
alidhamiria au la, lakini alinithibitishia kuwa alidhamiria kile alichokiandika
kwamba kitekelezwe,” amesema.
Mahmoud Mahinda,
Katibu Mtendaji wa JUVICUF Taifa, amesema matukio yanayoendelea kufanyika
Zanzibar yanafaywa kwa msaada wa CCM na kufafanua juu ya kundi la Mazombi
ambapo alidai kuwa ni vijana wa CCM waliowekwa katika makambi.
Aidha, JUVICUF
imeshangazwa na mkanganyiko wa viongozi visiwani humo ambapo Mkuu wa Mkoa wa
Pemba Kaskazini aliashiria hali ya hatari na kuamuru wananchi kujifungia ndani
inapojiri majira ya saa mbili usiku.
Taarifa hizo zinakuja wakati Charles Kitwanga, Waziri wa Mambo
ya Ndani ameshasemakuwa hali Zanzibar ni shwari na ulinzi uliohimarishwa na
kutaka kuwahakikishia wananchi usalama ili wajitokeze kupiga kura kwenye
uchaguzi wa marudio.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni