Zinazobamba

MAKONDA AANZA KAZI NA MIKWALA, AWATANGAZIA KIAMA WAUZA UNGA DAR,SOMA HAPO KUJUA



 

NA KAEOLI VINSENT 
JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, limefanikiwa kumkamata Kinara wa uuzaji wa dawa za kulevya jijini hapa aliyefahamika kwa jina la Hussein Halili 39, mkazi wa Mikocheni.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Kamishna Simon Sirro amesema mtu huyo amekamatwa kufuatiwa taarifa ilizotolewa na wasamalia wema ambapo jeshi hilo lilitega mtego na kumkamata Benson Charles (32), kwenye gari namba T 407 BMM, Toyota Hilux, aliyekuwa na dawa aina ya heroin kilo moja kwenye gari yake.

"Baada ya kumkamata katika mahojiano mafupi na Benson alisema kuwa mzigo huo si wake bali ni wa tajiri yake Halili ambaye walipanga kukutana maeneo ya Mbezi beach ili amkabidhi ambapo polisi waliongozana nae na hatimaye kumkamata kinara huyo," amesema.

Aidha amesema katika tukio hilo walikamatwa watu wengine wawili na kuweka wazi kuwa watu hao hawatatajwa majina yao kutokana na sababu za kiusalama na kwamba jeshi hilo linaendelea kufanya mahoajiano katika kuhakikisha linawakamata wengine wanaojihusisha na uuzaji wa dawa hizo.

Hivi karibuni Sirro kupitia vikosi vyake jijini hapa alitangaza msako makali wa kuwakamata wauza dawa hizo ambapo pia oparesheni hiyo iliwahusisha na mateja ili kuweza kuwafikia kwa urahisi wauzaji hao.



MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wamiliki wote wa silaha jijini hapa kuwasilisha taarifa ya uhalali wa silaha zao na kusajiliwa upya kwa wakuu wapolisi wa Wilaya (OCD).

Aidha amewataka watu wote wanao miliki silaha hizo kinyume cha sheria kuzisalimisha kabla ya kuanza kwa Oparesheni ya ukaguzi jijini hapa Julai mosi mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam leo wakati alipotembelea katika Kanda Maalum jijini hapa, Makonda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama jijini hapa, wamiliki hao wafike katika ofisi za wakuu wa polisi wa wilaya kuanzia April mosi mwaka huu hadi julai mosi mwaka huu itakapo anza oparesheni hiyo.

Amesema lengo la hatua hiyo ni kujihakikisha na kujua idadi ya silaha zinazotumika  na kuzisajili upya.

"Hivyo kwa yule ambaye hakutumia siku hizo katika kuwasilisha taarifa au kusalimisha silaha tutaona kwamba anatumia silaha hiyo kinyume na kile ambacho kilikusudiwa kwa utoaji wa silaha," amesema.

Hata hivyo alisema kwa wale ambao hawana nyaraka nao katika kipindihicho wasalimishe silaha hizo na kwamba mtu huyo hata chukuliwa hatua na kwamba silaha hiyo itachukuliwa na kuwekwa kwenye utaratibu unaostahili.

Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa jiji linaloongoza  kwa utulivu pamoja na kusitisha matukio ya ujambazi ya kutumia silaha, au pikipiki wala kusikia milio ya silaha na badala yake ni kuona jiji lina kuwa la amani na utulivu.

Makonda alitumia nafasi hiyo kulipongeza jeshi hilo na kuwatangazia utaratibu mpya wa kutoa tuzo kwa askari watakao pambana na ujambazi jijini hapa ambao wanawafanya watanzania wanaishi na hosfu katika kila kipindi cha miezi mitatu.

Alisema hatua hiyo ambapo skari bora atakao fanya vizuri katika pambana na ujambazi watapewa sh.milioni moja na mkuu wa mkoa huo ikiwa ni shemeu ya motisha na kuwatia moya katika kutimiza majukumu yao na katika hatua ya kupambana na ujambazi.

"Askari wanafanya kazi katika mazingira magumu katika kupambana na uhalifu hivyo kama mkuu wao wa mkoa hawezi kukaa kimya na kuona ni vyema kuweka fumo huo wa kuwaongezea motisha kwani hiyo ni kazi ngumu inayohitaji kutiwa moyo licha ya kwamba ni sehemu ya majukumu yao," alisema.

Kwa upande wake Kamanda Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro alisema kuna kila sababu ya kuhakiki silaha zote kwani matukio mengi yanayofanyika wakikamatwa watuhumiwa wanakutwa na silaha zinazokamatwa ni zile ambazo zilitolewa kwa umiliki kwa lengo zuri lakini inakuwa tofauti.

Hivyo baada ya miezi mitatu tutaanza oparesheni kubwa ya kuwakamata kwani tunataarifa za watu wote wanaomiliki silaha na kuwaomba Watanzania kujitokeza na si kusubiri kukamatwa lakini kama anaamini anatumia silaha hiyo inatumiwa kihalali ni vema kuiwasilisha na taarifa zake.

"Hivyo ni vema kuziwasilisha kwani hakuna haja ya kusubiri kukamatwa kwani mwishowake ni kufikisha mahakamani hivyo ni bora wafike katika sehemu elekezi kwaajili kuwasilisha taarifa zao na matumizi na kama umetumia risasi kumi ueleze katika hali gani," alisema

Hakuna maoni