RAIS MAGUFULI KUMWACHA MTUPU KIKWETE,SIRI NZITO ZAFICHUKA,SOMA HAPO KUJUA
John Magufuli, Rais wa Tanzania akiwa na Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania |
SERIKALI ya Rais
John Magufuli muda wowote kuanzia sasa inaweza kukamata maofisa waliofanya kazi
na Rais Jakaya Kikwete na kuwaburuza kortini, anaandika Happyness Lidwino.
Mkakati huo unaelekea kukamilika baada ya
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kufanya ukaguzi na
kujiridhisha kwamba maofisa 156 wanapaswa kufikishwa mahakamani.
Kati ya maofisa hao 156 kesi kubwa zinatajwa kuwa 98 ambapo
majalada 17 tayari yamepelekwa Biswalo Mganga, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai
(DPP) ili kupata kibali cha kuwaburuza mahakamani.
Takukuru kwa sasa wanasubiri kibali kutoka katika Ofisi ya
Mkurugenzi wa Mashitaka ili kuchukua hatua hiyo. Maofisa hao ni wale waliofanya
kazi na Rais Kikwete.
Kabla ya kubaini idadi ya maofisa hao wanaopaswa kufikishwa
mahakamani, Takukuru ilifanya ukaguzi 296 ambapo jumla ya majalada 252
yaliyofikishwa kwa DPP huku maofisa 156 pekee ndio walioonekana kuwa na sababu
ya kufikishwa mahakamani.
Hatua hiyo imebainika katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya
Utawala na Serikali za Mitaa kilichokaliwa tarehe 16 Machi mwaka huu ambapo
Valentino Mlowola, Mkurugenzi wa Takukuru alieleza kuwa, kinachosubiriwa kwa
sasa ni vibali.
Ukaguzi huo umefanyika katika kipindi cha miezi saba kuanzia
Julai mwaka jana hadi Januari mwaka huu.
Taarifa ya Mlowola kwa kamati hiyo ambayo mtandao huu inayo
inaeleza kuwa, tayari kesi mpya zimefunguliwa 208 katika mahakama mbalimbali
nchini huku kesi 113 watuhumiwa wake walipatikana na hatia.
Rais Magufuli wakati na baada ya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa
tarehe 25 Oktoba mwaka jana amekuwa akihubiri kuwachukuliwa hatua wabadhirifu
wa fedha.
Tayari maofisa kadhaa waliofanya kazi na Rais Kikwete ama
kuteuliwa wamefikishwa mahakamani kutokana na tuhuma za ufisadi hata hivyo,
mkakati zaidi uliopo ni kuhakikisha maofisa wengine wanapelekwa kujibu tuhuma
hizo ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Rais Magufuli kwa wananchi wake.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni