SAKATA LA KUTEKWA KWA MWANAHABARI WA DW NA GAZETI LA MWANANCHI ZANZIBAR,MAPYA YAIBUKIA KWA POLISI,SOMA HAPO KUJUATU
NA KAROLI VINSENT
WAKATI ikiwa haijulikani alipo mwanahabari Bi Salma
Saidi ambaye ni Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi na
shirika la Utangazaji la Ujerumani (DW) kutoka Zanzibar baada ya kutekwa na watu wasiojulikana
juzi maeneo ya uwanja wa ndege wa Mwalimu Juliasi Nyerere akitokea Zanzibar,
Tukio hilo imelifanya Baraza la Habari nchini (MCT)
kushirikiana na Mtandao wa watetezi wa haki za Binadamu Tanzania (THRDC),Jukwaa
la Wahariri nchini (TEF) Umoja wa
wanahabari Tanzania (UPTC) kuibuka na kuipa Jeshi Polisi siku nne Kuhakikisha
wanampata Mwandishi huyo wa habari lasivyo watakwenda mahakamani,
Kitoa Tamko hilo hilo leo Jijini Dar es Salaam kwa
niaba ya Taasisi hizo nne, mratibu wa
(THRDC) Onesmo Olenguruma wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo wao
kwa pamoja wanalaani tukio la kutekwa kwa mwandishi huyo.
Hata hivyo amesema mazingira ya kutekwa kwa
mwandishi huyo wanayafananisha na kazi yake ya habari kwani alipokuwa Zanzibar wakati anaripoti vizuri kuhusu hali ya uchaguzi wa marudio amedai kuwa alikuwa anakumbana na matatizo,
Olenguruma ameyataja matatizo hayo ni kwamba mara kwa mara wakati akiripoti
habari hizo alikuwa napigiwa simu mbali mbali na watu wasiojulikana walikuwa
wanampa vitisho,
“Kwa mazingira haya yote aliyokumbana nayo Bi Salma
yametokana na kazi yake,kwahiyo tunaiomba Jeshi la Polisi ndani ya siku
nne wawe wameshampata Bi Salma ,lakini kama watashindwa sisi tutakwenda
mahakamani ili tuiomba mahakama itoa hati kwa polisi kumtafuta Bi Salma awe
mzima au amekufa”amesema Olenguruma.
Kwa Upande wake Katibu Mtendaji wa (MCT),Kajibu
Mkajanga amesema hali ya Zanzibar sio salama kwa wanahabari kutakana na hali
misuguano inayoendelea visiwani humu huku akiwataka waandishi wa habari wawe
makini.
Naye Theophil Makungu ambaye ni mwenyekiti wa Jukwaa
la wahariri amesema kwa sasa wanalisihi jeshi la Polisi kuhakikisha wanamwokoa mwanahabari huyo kutoka kwa watu waliomteka.
MAZINGIRA YA
KUTEKWA YALIVYOKUWA,
Mwandishi wa Habari wa Radio Deutsche Welle(DW-Swahili), Salma
Said jana alikamatwa na watu wasiojulikana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Abeid Amani Karume mjini Unguja, alipokuwa akisafiri kwenda Dar es Salaam
kwa ajili ya kuangalia afya yake.
Akizungumzia tukio hilo jana, mume wa Salma, Ali Salim Khamis
ambaye pia ni Mbunge wa Mwanakwerekwe (CUF), alisema alipata ujumbe wa
maandishi kutoka kwa mkewe kwamba amekamatwa.
Khamis alisema alipokwenda uwanja wa ndege aliambiwa na mkuu wa
polisi wa uwanjani hapo kwamba hana taarifa za tukio hilo jibu ambalo alilipata
pia kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mjini Magharibi.
Alisema aliamua kwenda kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa ambako pia
aliambiwa hawana taarifa za kukamatwa kwa Salma. “Hadi sasa sijui mke wangu yuko wapi bado naendelea kumtafuta.”
Khamis alisema Salma alikuwa tayari amepitia taratibu zote na
alikuwa akisubiri kuingia ndani ya ndege ambayo haikutajwa, lakini alisema
ndege hiyo iliyokuwa iondoke saa 8.05 mchana ilizuiwa na watu hao wanaodaiwa
kuwa ni askari hadi saa tisa kasoro, walipoiruhusu lakini ikidaiwa kuwa
waliondoka na Salma kwenda kusikojulika
Hakuna maoni
Chapisha Maoni