Zinazobamba

JANUARY MAKAMBA APONI KABISA,MADUDU YAKE YATINGA MIKONONI MWA MAGUFULI,NI SAKATA LAKE KWENYE UDALALI,SOMA KUJUA







NI Mungu tu ndiyo anaweza kumwokoa  JANUARY Makamba ambaye  ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na mazingira) kubaki kwenye Nafasi hiyo ndivyo naweza kusema baada ya madudu yake kumfikia Rais John Magufuli,(Mtandao huu umeelezwa)Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo,

Makamba ambaye ni Kada wa Chama cha Mapinduzi CCM ameingia kwenye Kashfa kubwa ambayo imitikisa nchini kwa sasa,baada ya kuhusishwa kwenye udalali wa miradi kadhaa ya serikali kwa lengo la kujipatia Fedha,

Miradi hiyo ambayo haikutajwa wazi ,lakini January anahusishwa katika sakata la Mwekezaji wa Kitaliano ambaye amekuwa nchini kwa mda wa miaka mitano sasa ,akifanya Mapenzi na Mwamvita ambaye ni Dada yeke January,huku akitumia nafasi hiyo kupanga mikakati ya kujenga mahusiano na viongozi wandamizi wa serikali,

Kwa mujibu wa Taarifa ambazo Fullhabari.blogs imezipata toka ndani ya Ikulu zinasema Teyari sakata hilo limemfikia Rais magufuli na sasa amekuwa akilichunguza kwa makini ili kujilidhisha na kuchukua hatua kali kama alivyochukua kwa Aliyekuwa Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue ambaye naye alikuwa na tuhuma lukuki.

“Yaani nakuapia ndugu Mwandishi teyari suala hili limeshafika kwa Magu (Magufuli)Tangu Gazeti la Mtanzania lilipoandika siku ya kwanza,yaani mwenyewe  Rais amefedheheshwa na ameona akilifumbia macho suala hili litauchafua utawala wake ambaye yeye amepaaka kupambana na Mafisadi,nakuhakikishia kama Magufuli akibaini kama jambo hili linaukweli basi January aponi”ametupasha mtoa taarifa wetu huyo,

Kabla ya Taarifa hizi za Udalali wa January kwenye mali za Umma kwa watu wanaoitwa ni wawekezaji azijamfikia Rais Magufuli zilianza kuzagaa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Mitandano ya Kijamii,

Ambapo Taarifa hizo kwenye mitandao ya kijamii inamtaja January kuwa ni mmoja wa Mawaziri wa awamu ya nnewaliotumiwa na mpiga dili huyo,ingawa waziri huyo mwenye Hulka ya Kiburi amekuwa kipinga suala hilo,

Kinachoitwa “Udalali wa January” ni Mange Kimambi,mmoja wa makada wa CCM ambaye amefichua siri hiyo anasema Mpiga dili huyo wa Kitaliano anaishi kwenye Hoteli moja kwa miaka mitano ambayo inaelezwa kuwa alimpatia January Bilioni moja kwa ajili ya kupewa tenda serikalini,

Sauti na jumbe mbalimbali zilizosambazwa na kuwekwa kwenye mtandao na mtu maarufu kwenye mitandao ya kijamii na mmiliki wa tovuti ya U-Turn, Mange Kimambi, raia wa Tanzania aishie Marekani, zinaonesha mazungumzo kati ya watatu hao, mwaka 2011. Jana, Mwamvita na Makamba walikiri kuwa sauti hizo ni za kweli.

Muitaliano huyo ambaye anadaiwa kumpa Mange Kimambe ushahidi wote wa mawasiliano kati yake na Ndugu hao, amejitokeza na kuwasafisha akidai kuwa hakuwahi kuwapa rushwa wala kuhusiana na January kibiashara.

Cozzolino ameandika ujumbe akidai kuwa ingawa yeye na Mwamvita walikuwa na uhusiano wa mapenzi mwaka 2011 na baadae kujiingiza katika biashara binafsi ambayo ilipelekea kugombana kwao, hawakumhusisha January kwa aina yoyote katika biashara yao.

“Sikuwahi kumuomba [January] kunisaidia katika biashara zangu. Sikuwahi kumpa fedha. Mara chache nilizokutana naye ilikuwa ni mazungumzo ya kawaida ya kijamii. Nilikuwa na uhusiano na Mwamvita. Uhusiano wetu ulikuwa bomba mwanzoni lakini ukawa na mwisho mbaya,” ameandika Cozzolino.

Awali, sauti ya January na mwandishi wa habari iliyosambazwa, January anasikika akieleza kuwa aliwahi kukutana mara moja Dubai na Muitaliano huyo na kwamba alitambulishwa kama mpenzi wa dada yake. 

Alisema baadae dada yake alimwambia wameanza kufanya biashara ya kahawa na Muitaliano huyo na baadae biashara hiyo kufa huku ikiwaacha katika mzozo. 

Kwa mujibu wa Kamamba, Muitaliano aliyekuwa ameweka nusu ya mtaji ambayo ni dola milioni 50, alianza kudai kiasi hicho cha fedha na sio vinginevyo. 

Alisema kuwa awali, muitaliano huyo alikuwa anajaribu kumshawishi Mwamvita amkutanishe na viongozi wakubwa wa serikali ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu.

Hata hivyo, Mange Kimambe ambaye ndiye anayeeleza kuwa na nyaraka zote za ushahidi aliokabidhiwa na Muitaliano huyo na kwamba hivi sasa Muitaliano amelipwa na kukubaliana kumsafisha Mbunge huyo wa Bumbuli.

Mange amesisitiza kuwa ana ushahidi wote wa January na dada yake kupokea rushwa kutoka kwa mfanyabiashara huyo na yuko tayari kuwakabidhi Takukuru.

Hakuna maoni