Zinazobamba

GAZETI LA DIRAMTANZANIA LAMFUKIZISHA KAZI YULE WALIOMUITA JIPU LILOKUWA LINAKAA IKULU YA MAGUFULI, AMBAYE NI OMBENI SEFUE,SOMA HAPO KUJUA



 

NA KAROLI VINSENT
WIKI moja kupita baada ya Gazeti la DiraMtanzania   kuandika taarifa inayoitwa ni madudu na Gazeti hilo juu ya  Katibu Mkuu Kiongozi,Ombeni Sefue aliyokuwa anafanya katika Ikulu ya Rais John Magufuli,ikiwemo kuwapa vyeo watu wasiokuwa na sifa pamoja na kuzipa tenda mbali mbali kampuni zisizo na sifa,

Taarifa hiyo iliyochapishwa kwenye Gazeti hilo ambayo iliyoambatana  na Makala iliyomuita Sefue kuwa ni Jipu lilokuwa linakaa Ikulu,Hadi Taarifa hiyo iliyopelekea Serikali kulitaka Gazeti hilo kuomba Radhi kwa kiongozi huyo kwa kudai Taarifa hizo zote ikiwemo  Makala zilizomuhusu Sefue ni za uongo,

Wakati Gazeti la Diramtanzania likisubiliwa na wananchi mbali mbali kujua kama litaomba Radhi au la,Hatimaye ndivo tunaweza kusema Labda kilio cha Gazeti hilo  kimemfikia Rais Magufuli hadi mpaka kufikia hatua ya  kumwondosha Sefue  katika nafasi aliyekuwanayo Katibu huyo kiongozi na kumtafutia nafasi nyingeni.
Kwa mujibu ya Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu,Gerson Msigwa kwa vyombo vya Habari inasema  ambayo bila ya kutaja sababi ya Sefue kutolewa kwenye Nafasi hiyo inasema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemteua Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. 

Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Kijazi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India. Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue atapangiwa kazi nyingine.


Hakuna maoni