MBUNGE WA CCM ATAKA SERIKALI IRUHUSU WATANZANIA WAVUTE BANGI NA KULA MIRUNGI,SOMA HAPO KUJUA
Mbunge wa Geita vijijini kwa tiketi ya CCM, ndugu Joseph Kasheku (Msukuma) ameishauri serikali kuruhusu kisheria kilimo cha Bhangi na Mirungi ili kuiwezesha kujipatia fedha za kigeni kutokana na mauzo ya mazao hao
Mbunge huyo aliyasema hayo jana katika kikao cha 5 cha bunge la 11 linaoendelea na vikao vyake katika ukumbi wa bunge mjini Dodoma.
''Mheshimiwa mwenyekiti zao la mirungi na bhangi kuna nchi zinaruhusu .Mfano mzuri mfano ni majirani zetu wa Kenya ambao ndege mbili kubwa hutua nchini humo kuchukua mirungi na kupeleka ulaya,sasa kwa nini sisi tusiendeleze zao hili linalopatikana Geita na maeneo ya Bunda mkoani Mara na maeneo mengine nchini ili wananchi wanufaike kwa kuuza zao hilo ?'' Alihoji Msukuma na kuongeza;
"Kwa wasukuma kule kwetu mtu akitumia bhangi anapata nguvu ya kulima sana hata hekari mbili lakini inakatazwa na wakati huo huo vijana wetu tumewaruhusu kutumia viroba ambavyo huwadhoofisha sana pengine kushinda hata bhangi, naomba tufanye utafiti upya juu ya hili.
"Wapo wenzetu humu (wabunge) wanaitumia bhangi na hakuna madhara yoyote, tena wanachangia hoja kwa ufasaha kabisa."
Baada ya hoja hiyo ya Mbunge Msukuma, Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Khamis Kigwangalla alisimama kumjibu ambapo alisema madawa ya kulevya aina ya bhangi na mirungi yana athari kubwa sana za kiafya na hasa afya ya ubongo .
Kingwangalla alisema serikali kwa namna yoyote haitakubali kuruhusu au kujadili kuhalalishwa kwa madawa hayo
Hakuna maoni
Chapisha Maoni