Zinazobamba

BENKI YA CRDB YAWATOA HOFU WATEJA WAKE,SOMA HAPO KUJUA





SIKU moja baada ya Serikali kutangaza kuchukua hatua za kupunguza riba za  mabenki kwa wananchi kwa kuagiza akaunti za mashirika na taasisi zake  katika mabenki ya kibiashara zifungwe na kuhamisha fedha zilizopo katika akaunti hizo kwenda Benki Kuu ya Tanzania (BoT), benki ya CRDB imeunga  mkono hatua hiyo.
  Pia benki hiyo imewataka wananchi wasiwe na hofu juu ya mpango huo,  kutokana na hofu iliyojengeka kwamba kuna hatari benki za kibiashara  kufilisika nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei alisema uamuzi uliofanywa na Serikali utasaidia kukuza uchumi pamoja na kutambua fedha zake mahali  zilipo.

Alisema Serikali ina haki na nia njema kwa kutaka akaunti hizo zifunguliwe BoT  kwa kuwa zimekuwa zikifunguliwa kwenye mabenki makubwa ya kibiashara,  huku baadhi ya Wakala wa ukusanyaji wa fedha wakishindwa kuzifikisha  serikali kama inavyotakiwa.

Pia alieleza kuwa mfumo huo hauna utofauti na awali kwani utofauti  utakuwepo kutokana na mashirika na taasisi kufungua akaunti BoT, ambapo  lengo kubwa ni walaka wa Hazina kulenga kuboresha mapato ya serikali  ammbayo yanaweza kutumiwa kwa namna mbalimbali.
“Mfumo huu…utakuwa hauna tofauti na ilivyo sasa kwa kuwa fedha zitakazokuwa  zikiingizwa kwenye akaunti hizo ni zile zilizokuwa zikiingizwa kwenye  benki awali, ili kupunguza kiwango cha riba,”alisema.

Pia alisema hofu nyingine inayojengeka kwa wananchi inatokana na mfumo huo kutotumiwa kwa muda mrefu na BoT, licha ya kuwa kuna baadhi ya nchi
inatumia mfumo huo na hakuna madhara yoyote.

“Hivyo tunafikiri maamuzi hayo hayana athari zozote kwani nchi mbalimbali  zimekuwa zikitumia mfumo huo ikiwemo Uganda, Rwanda na Kenya ila kwa  kwetu unaonekana mgeni kutokana na kutotumika kwa muda mrefu,”alisema.

Pia Dk.Kimei Amesema kuwa kutokana na uwepo wa mfumo huo benki za kibiashara zitawakopesha zaidi sekta binafsi, ikiwa tofauti na malalamiko ya mwanzo kwamba Serikali inapata manufaa kutokana na kukopeshwa zaidi.
“Hii itasaidia hata wananchi wa kiwango cha chini kuchukua mikopo kutokana  na riAba kuwa ndogo, ambapo hata wananchi wa chini wataweza kuchukua  mkopo, ikiwa tofauti na awali wananchi wanashindwa kuchukua mikopo kutokana na riba kuonekaa kuwa juu zaidi ya asilimia 10,”alisema.

Mbali na hilo, pia Kimei alisema endapo riba ikiwa inapungua itasaidia kukuza
uchumi kutokana na wananchi wengi wa hali ya chini kuchukua mikopo.
 
A

Hakuna maoni