Zinazobamba

BAKWATA NAO WAINGIA KWENYE MKUMBO WA JECHA WA ZEC,WAIBUKA NA KUWATAKA WAISLAM WASHIRIKI MARUDIO YA UCHAGUZI,SOMA HAPO KUJUA

 pichani ni 
Sheikh Mkuu mkoani hapa,Sheikh Alhad Mussa Salum akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam,

NA KAROLI VINSENT
WAKATI Chama  cha wananchi CUF,ambacho ni chama kikuu cha Upinzani visiwani Zanzibar kikiwa kimesusia uchaguzi wa marudio ambao unafanyika Marchi 20 ya mwaka huu,nalo Baraza la Waislam nchini (BAKWATA) limesema marudio ya  uchaguzi huo ni njia ya kipee ya kurudisha amani visiwani humo..
.
Hata hivyo,Bakwata limeitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar,(ZEC) kutenda haki katika uchaguzi huo wa marudio.

Kuibuka huku kwa Bakwata kuna kuja ikiwa ni wiki tatu kupita baada ya Jumuiya ya Maimamu visiwani Zanzibar kupinga hatua ya ZEC ya kutangaza  marudio ya uchaguzi huo kwa madai utaleta mgawanyiko mkubwa visiwani humu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo,Jijini Dar es Salaam,  amesema  Bakwata wanaunga mkono Tangazo la ZEC la kurudiwa kwa uchaguzi huo  wa marudio.
“Uchaguzi huu wa marudio  kwetu Bakwata tunaona ndio njia ya kipekee ya kukiweka kisiwa cha Zanzibar kuwa sehemu ya Amani na utulivu,natumia nafasi hii kuwoamba chama cha CUF kushiriki uchaguzi huu”Amesema Sheikh Salum,

Sheikh Salum ameongeza kwa kusema  kuwa hata kiongozi wa jumuiya ya Uamsho Visiwani Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmad amemuandikia barua kwa kumweleza kuwa kurudiwa kwa uchaguzi kutasaidia kurudisha Amani visiwani humo.

Katika Hali ya kushangaza mara baada ya Waandishi wa habari walipomtaka Sheikh Salum kuonyesha barua hiyo aliyotumiwa na Sheikh Faridi aliyotumiwa,ndipo Sheikh Salum akaonyesha barua hiyo,ambapo barua hiyo ilikuwa ajaandikwa Anuani wala tarehe jambo lilozidi watia shaka waandishi wa habari.
Mwandishi wa Mtandao huu alimtafuta Sheikh Farid kutaka kujua juu ya ukweli wa barua hiyomndipo simu yake ilikuwa aipatikani.



Hakuna maoni