TRL YASITISHA SAFARI ZAKE ZA DAR NA KUHAMISHIA MKOANI DODOMA, SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Afisa Habari wa TRL,Midraji mahezi akizungumza na waandishi wa habari le,Jijini Dar es Salaa |
KAMPUNI ya
Reli nchini (TRL)imetangaza kuhamisha huduma zake za usafirishaji kutoka
mkoani Dar es Salaam hadi mkoani Dodoma kutakana na Tatizo la miundomi ya Reli
iliyoaribika kutokana na Mvua kubwa
zilizonyesha hivi karibuni mkoani Morogoro.Anaandika KAROLI VINSENT
endelea nayo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam afisa habari wa TRL,midraji Mahezi kwaniaba ya Kaimu mkurugenzi mtendaji wa TRL,,Mhandisi
Elias Mshana, amesema TRL wamefikia hatua hiyo ili kupisha ukarabati wa tuta la
reli lilopo kati ya stesheni za Kidete na Kilosa zote mkoani Morogoro.
“Kutokana na Mafuriko ya eneo la Kidete na Kilosa
kutojulikana lini yataisha ,uongozi
umeamua kwa sasa kusitisha zoezi la ukarabati ili kuokoa rasilima zilizotumika
katika eneo hili,hata hivyo kazi ya kuzuia uharibifu zaidi dhidi ya tuta la
reli inaendelea kulingana na hali inavyojitokeza”amesema Mahezi.
Mahezi,amefafanua kwa kusema kuwa japo hatua hiyo itaongeza
gharama lakini amedai kuwa ni muhimu kwa huduma za usafirishaji ziendelee ili kuwasaidia watanzania kiuchumi na kijamii kadri
inavyowezekana akieleza kuwa huduma ya reli inapunguza kasi ya uharibifu wa
barabara zetu ambazo sio mda mrefu zimejengwa kwa gharama kubwa,
Hata hivo,Mahezi
amewaomba radhi watumiaji wa huduma hiyo kwa kuwataka kuwa wavumilivu mpaka
huduma hiyo itakaorejeshwa tena mkaoni hapa,
Vilevile,Mahezi amesema uzoefu unaonyesha kuwa sio
mara ya kwanza kusitisha huduma hiyo kwa madai kuwa katikakiindi cha mwaka 1998
na 2010 huduma za reli zilihamia mkoani Dodoma ,wakati viindi hivyo maeneo ya
Kidete na Kilosa yalipokutwa na mafuriko kama ya mwaka huu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni