DK SLAA AZIDI TEKETEA KIMAISHA,MCHUMBA WAKE AMUINGIZA MATATIZO TENA,SOMA HAPO KUJUA
pichani ni aliyewai pata kuwa Katibu mkuu wa Chadema,DK Slaa |
MCHUMBA wa aliyewahi kuwa,Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo Chadema,Jospehine Mushumbusi amezidi mwingiza matatizoni ,Dk Wilbroad
Slaa baada ya kusababisha nyumba yake kuuzwa ,(Fullhabari.blogs imebani),Anaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Dk Slaa
ambaye alitanga uamuzi wa kujiuzulu kwenye nafasi hiyo ndani ya Chadema semtemba mwaka jana kwa
kisingizio cha kutoridhishwa na ujio wa Edward lowassa ndani ya chama hicho,ambapo
kwa sasa taarifa zilizopatikana zinasema Nyumba ya Dk Slaa imeuzwa kwa mnada
kutokana na deni alilokopa Mchumba wake huyo kwenye Taasisi moja ya kifedha
hapa nchini.
Taarifa za
kuaminika ambazo mtandao huu umezipata zinasema Nyumba hiyo iliyoko mtaa wa
mtipwa,Mbweni jijini Dar es Salaam,imeuzwa kwa mnada kama mithili isiyokuwa na
mwenyewe,
Fullhabari
imedokezwa kuwa mchumba wake huyo alikopa milioni 300 miaka michache iliyopita
kwenye Taasisi moja ya kifedha ambayo (jina tunaliifadhi) iliyoko maeneo ya
Mlimani City jijini hapa.
Taarifa za kiuchunguzi ambazo mtandao huu umezifanya
zinaonyesha Nyumba hiyo ambaye alijengewa na Mwenyekiti wa Chadema,Freeman
Mbowe ,inaelezwa kuwa Nyumba hiyo
imenunuliwa na Tajiri mmoja kijana
ambaye amekuwa akijihusihwa kufadhili Bendi za Dansi nchini.
Wakithibitishwa kuuzwa kwa nyumba hiyo,majirani wa
Dk Slaa,wameumbia mtandao huu kuwa Nyumba hiyo imeuzwa na wao wameshuhudia.
“Ni kweli ndugu nyumba hii imeuzwa kwa mnada maana
mnada wake ulitangazwa na inavyoonekana huyu Slaa alipewa mda lakini alishindwa
kulipa sasa sahivi sio yake tena”amesema Jose Elias jirani wa Dk Slaa.
Taarifa ambazo zimezagaa zinasema kwa sasa Dk Slaa
ametelekezwa na wale waliomshawishi akihujumu Chadema.
‘Huyu bwana (Slaa) wakati alipokuwa Chadema
alitusakama sana watu wa TISS,alizushia maneno ya uongo,na sahivi tunafurahi
ametoka kule amekuwa upande wetu ila,na sahivi hatuna habari naye atajua
mwenyewe ”
Taarifa za kuuzwa kwa nyumba hiyo,kuna kuja ikiwa
kuna taarifa kuwa Dk Slaa hayupo nchini kwa sasa yupo nchini Canada kwa mambo
yake ya kikazi,taarifa hiyo inadai kuwa mara baada ya Dk Slaa kusikia Nyumba
yake hiyo kuuzwa ammtuma mchumba wake huyo na mda wowote atarejea nchini na
kujakufungua kesi mahakamani kupinga uuzwaji nyumba hiyo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni