TIZAMA TASWIRA NZIMA KATIKA BUNGE LEO,PIA TUNDU LISSU NAYE AANZA MAKEKE YAKE AIBANANISHA SERIKALI BUNGENI,SOMA HAPO KUJUA
Spika
wa Bunge Job Ndugai (kulia) akimwapisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa , bungeni mjini Dodoma Januari 26,
2016.
Spika
wa Bunge Job Ndugai (kulia) akimwapisha Waziri wa Fedha na Mipango,
Dkt.Philip Mpango, bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.
Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na
Walemavu, Dkt. Abdallah Possi akijibu maswali Bungeni Mjini Dodoma
Januari 26, 2016.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu,
Jenista Mhagama akijibu swali Bungeni Mjini Dodoma Januari 26, 2016.
Wabunge wakisikiliza hoja mbalimbali bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.
Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na
Walemavu, Anthony Mavunde akijibu maswali Bungeni Mjini Dodoma Januari
26, 2016.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa hoja ya kutaka Bunge lijadili Hotuba ya
Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati alipofungua Bunge
la Kumi na Moja Novemba 20, 2015.
Mbunge wa Mvomero, Murad Sadiq akichangia bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.
SERIKALI imeshindwa kutoa majibu yanayoeleweka baada
ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) kutaka kujua ni lini
serikali itakamilisha ahadi yake kwa kupeleka madawati 708 yaliyotokana na
chenji ya rada katika kila wilaya. Anaandika Danny Tibason, Dodoma …
(endelea).
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imeshindwa kutoa majibu hayo kuhusu ahadi ya
serikali ya kusambaza madawati kama ilivyoahidi.
Lissu
alisema kuwa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambako pia kulikuwa na
ahadi ya aina hiyo, hakuna hata dawati moja ambalo lililopelekwa na hajui mpango
huo uliishiwa wapi.
Awali
serikali iliahidi kupeleka madawati kwa baadhi ya halmashauri za wilaya ambayo
yangepelekwa kila wilaya madawati 708 ambayo madawati hayo yalikuwa katika
muundo wa plastiki.
Akijibu
swali hilo, Waziri wa Nchi, Tamisemi, George Simbachawene amesema kuwa mpango
huo bado upo na kwamba, kuna shule ambazo zilipelekewa madawati kama
ilivyotakiwa.
Hata
hivyo amesema kuwa atapitia kuangalia ahadi katika baadhi ya maeneo ikiwemo
kupeleka bungeni mkakati maalumu wa Serikali ya Awamu ya Tano utakaohakikisha
kuwa tatizo la madawati kwa Shule za Msingi na Sekondari linakwisha.
Katika
hatua nyingine, serikali imetoa nafasi kwa baadhi ya wazazi na wadau wengine
kuchangia michango katika upatikanaji wa madawati kwa kadri watakavyoona inafaa
ilimradi wasisumbue au kufanya michango hiyo iwe kizuizi cha kupeleka watoto
kuendelea na masomo.
Kauli
hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayasnsi, Teknolojia na Ufundi, Stella
Manyanya wakati akijibu swali la Mbunge wa Ndanda, Cesil Mwambe (CUF).
Mbunge
huyo alitaka kujua serikali imejipanga vipi kuhakikisha wanafunzi hawarudishwi
shule kwa sababu ya michango ya mlinzi, madawati na chaki.
Naibu
waziri amesema kuwa hakuna mkuu wa shule yeyote ambaye atamrudisha mwanafunzi
nyumbani kwa kutolipa michango ya mlinzi, madawati na chaki kwa sababu ya
majukumu hayo ni ya Serikali.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni