TAASISI YA KARIMJEE YATOA TUZO ZA WANASAYANSI CHIPUKIZI,SOMA HAPO KUJUA
pichani ni washindi wa jumla wa tuzo za wanasayansi chipukizi za young Scientinsts wakikabidhiwa vyeti |
NA KAROLI VINSENT
KATIKA kuinua sekta ya sayansi nchini,Taasisi ya
Karimjee Jinavanje imewatunuku nafasi za masomo Edmound Luguku na John
Method wanafunzi wa shule ya sekondari
ya mzembe kuwa washindi wa jumla ya tuzo za wanasayansi chipukizi za
Young Scientinsts Tanzania kwa mwaka 2015.
Hayo yametokea leo jijini Dar es Salaam wakati wa halfa
fupi ya kuwaaga washindi hao,ambapo
akiongea na wanahabari wakati wa halfa hiyo,Meneja wa taasisi hiyo,Devotha
Rubuma amesema washindi hao wawili walipata fursa ya kupelekwa masomoni baada ya kumaliza
kidato cha sita.
Ameeleza kuwa washindi watasafiri leo kuelekea
Dubiln nchini Ireland ambapo watahudhuria maonesho ya kimataifa ya sayansi na Teknolojia ambapo
kila mwaka hufanya mashindano
yanayolenga kuhamasisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kupenda
sayansi,
Kwa upande wake mwenyekiti wa heshima ya kundi la
makampuni ya KarimjeeJivanje,Hatim Karijee amesema tuzo lengo la shindani hilo
ni kutoa uwezo kwa watanzania,
“Tumepewa heshima kubwa sana kuweza kuwa sehemu ya
tuzo za Young Scientist Tanzania kwani tunaamini kwamba elimu ni muhimu sana
kwa mustakabali wa maendeleo ya Tanzania na pia kwa sababu elimu ya sayansi
inaweza kuleta fursa nzuri
kitaalum”amesmea Karimjee.
Karimjee ameongeza kuwa lengo la kimtazamo wa taasisi hiyo hivi
sasa ni kuisadia taasisi za elimu kwa
kuboresha uwezo wake,familia ya karimjee ilianisha taasis mbali mbali za
misaada kwenye miaka ya 1950 kabla ya uhuru.
“Tumejenga shule nyingi ,hospitali ,zahanati na
vituo vya huduma za kijamii ambazo
mojawapo ya misaada wetu mkubwa ni ukumbi wa mkubwa wa Karimjee ambazo tuliujenga ambao
tulilenga na kuutoa msaada kwa
Halmashauri ya Manispaa ya Dar es salaam mwaka 1957”
Hakuna maoni
Chapisha Maoni