Zinazobamba

SERIKALI YAWATANGAZIA KIAMA WAHUJUMU UCHUMI,SOMA HAPO KUJUA

 

1.Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna Diwan Athuman akisoma taarifa yake.-001
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna Diwani Athumani, akisoma taarifa.

Serikali inaendelea kusimamia urejeshaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya kihalifu kupitia mpango wa  kupambana na uhalifu ulioanzishwa mwaka 2012 kwa kuwashtaki na kuwataifishia mali zao pindi upelelezi ukikamilika na kubainika mhalifu ana makosa hayo.Baadhi ya watuhumiwa kadhaa wamepelewa mahakamani na kufungwa, ikiwemo mali zao kutaifishwa na kuwa mali ya Serikali.

   Hayo yalisemwa na  Mkurugenzi wa Mashtaka nchini ( DPP) Biswalo  Mganga wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ofiisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi   jijini Dar es salaam, ambapo  alisema kuwa hatua hizo zimechukuliwa mara baada ya  upelelezi wa makosa ya kuhujumu uchumi kukamilika na kumbaini mhusika.
   Aidha Mganga aliongeza kwamba  mhusika  hushtakiwa na mali zake kutaifishwa kulingana na kosa lake, pia suala hili litamgusa kila mtu, wakiwemo  watumishi wa umma.

“Mhalifu wa kuhujumu uchumi wa nchi ikiwemo usafirishaji wa nyara za Serikali, uuzaji wa madawa ya kulevya na kujipatia mali kwa njia ya rushwa watatumikia adhabu ya kulipa
faini, kufungwa jela na kutaifishiwa mali zake pindi atapobainika na makosa hayo” alisema  Mganga.


Alisema kufuatia mkakati huo, Jeshi la Polisi limekamilisha upelelezi wa kesi 23 ambazo ziliwasilishwa kwa DPP na kati ya hizo tatu (3) zimetolewa uamuzi na nyingine ishirini (20)
ziko katika hatua ya maombi ya kupata amri ya mahakama ili ziweze kuziwa au kutaifishwa.
Alizitaja baadhi ya kesi za dawa za kulevya ambazo zimefikia ukomo na kutolewa uamuzi Januari 27, mwaka huu.Mkoani Kilimanjaro kesi mojawapo ni Josephine Waizela, ambaye ni raia wa Kenya aliyetiwa hatiani  kwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Cocaine  zenye uzito wa kilogram tatu zikiwa
na thamani ya Sh. Milioni 162 na kufungwa kifungo cha maisha.
Kesi nyingine ni namba 46 ya mwaka 2014 kutoka pia mkoani Kilimanjaro ambayo ilihusisha watu watatu, mmoja kati yao ambaye ni Hamis Mbwana alitiwa hatiani kwa kukutwa na dawa za kulevya aina Heroine zenye uzito wa gram 3191.11 na thamani ya Sh. Milioni 143, watuhumiwa wengine wawili katika kesi hiyo waliachiwa huru.


Mganga alizitaja baadhi ya kesi nyingine za uhujumu uchumi ni namba 6 ya mwaka 2015, ilisikilizwa mkoani Mbeya ambayo iliwahusisha raia wanne kutoka nchini China waliotiwa hatiani kwa kosa la kukutwa meno ya vifaru 11. Raia hao ni  Song Lei , Xiao Shaodan, Chen Jianlin na HU Liang, ambao wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 na kulipa faini ya Sh. Milioni 9,288 kwa kila mmoja.
Kesi nyingine  ya uhujumu uchumi namba 3 ya mwaka 2016
iliyomhusisha raia wa Tanzania Amani Rashid Ngaza aliyetiwa hatiani  kwa  kosa la kukutwa na meno ya tembo nane  iliyosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
mkoani Katavi, wilaya ya Mpanda. Mtuhumiwa huyo amefungwa kifungo cha miaka 30
na kullipa faini ya Sh. bilioni 1.2.
Katika mkutano huo, Mkurugenzi Maganga alibainisha baadhi ya mali zilizotaifishwa kutoka kwa wananchi kuwa ni magari matano aina ya Toyota Rv 4 mbili ,Suzuki, Toyota Surf ,
Hiace pamoja na nyumba  kutoka kwa washtakiwa mbalimbali wa makosa ya kuhujumu uchumi.

Aidha,  Mganga alitoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano bila uwoga katika kufichua mali za mafisadi ili sheria ichukue
mkondo wake pamoja na kuwataka wananchi wasijihusishe kwa njia yoyote ile ili kuficha umiliki wa mali ya mtu mwingine aliyoipata kiharamu kwa nia ya kuficha uhalifu wake kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.
“Kwa mujibu wa Sheria aliyeshirikikuficha mali ya mtu mwingine inayohusiana na uhalifukwa njia yoyote
ile pia anaweza kushitakiwa kama aliyetenda kosa la ufisadi,” alisema.
     Kwa upande wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Kamishna Diwani Athumani alisema
kuwa atakayekamatwa na kosa la wizi au mali ya haramu atatumikia adhabu na mali zake kutaifishwa.“Mhalifu akibainika namshataka ya wizi au kujipatia mali kwa njia ya haramu atatumikia adhabu na
kutaifishiwa mali zake kama vile magari, nyumba, boti, viwanja na fedha taslimu”
alisema Kamishna Athumani.
Aidha, Kamishna Athumani aliongeza kuwa uzoefu wao unawaonyesha kwamba wahalifu wanatumia majina ya wake
zao, waume zao, watoto wao na wakati mwingine kutumia majina ya watu ambao hawapo ili kuendelea kufaidika na mali walizozipata kwa niia za uhalifu.
 “Hakuna mhalifu atakayepona katika mapambano haya pia uhalifu haulipi na hauna nafasi nchini” alisistiza
Kamishina Athuman.

 Mbali na hayo, Mkurugenzi wa upelelezi Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) Alex
Mfungo pia alisema kuwa wameanzisha kitengo cha kutaifisha mali zilizopatikana kwa njia ya uhalifu ikiwemo rushwa.

Tangu mwaka 1990, Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ilitambua utaifishaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya kihalifu
kama kipaumbele katika mfumo wa haki jinai wa kupigana na uhalifu.  Haisadii sana katika jitihada za kupambana na
uhalifu ikiwa mhalifu atapata adhabu ama ya kutozwa faini au kwenda jela ikiwa
ataachiwa uhuru na kupewa fursa ya kutumia fedha au mali iliyopatikana kwa
uhalifu huo.


Zaidi, fedha zilizoibwa na wanasiasa wala rushwa
pamoja na wahalifu wengine, zinahitaji kutaifishwa na kuelekezwa katika maeneo
muhimu yenye mahitaji.

Sheria ya Utaifishaji wa Mali Haramu ilipitishwa
na Bunge mwaka 1991 ili kuendana na muelekeo wa Kimataifa pamoja na mikataba ya
Kimataifa ambayo imeridhiwa na nchi yetu.

















Hakuna maoni