RAIS MAGUFULI NA WAZIRI LUKUVI WAIFANYIA UNYAMA HOTELI YA GOLDEN TULIP,SOMA HAPO KUJUA
Baadhi ya wafanyakazi wa Hoteli ya Golden Tulip
wakiendelea na zoezi la uondoshaji wa mabati yaliyoweka kama uzio katika eneo
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi akizungumza na waandishi wa habari waliokuwepo kwenye eneo hilo.
Msafara wa Rais Dkt. Magufuli ukipita wakati zoezi la kuuondoa uzio wa
Hoteli ya Golden Tulip likiendelea.
SERIKALI imevunja uzio wa eneo la maegesho ya magari
wa hoteli ya Golden Tulip Jijini Dar es Salaam kutokana na umiliki wa
eneo hilo kutolewa kwa njia zisizo halali.Hatua hiyo imefikiwa baada ya
Serikali kushinda kesi dhidi ya mmiliki wa hoteli hiyo.
Kazi ya kubomoa uzio huo imefanywa kwa ushirikiano wa Baraza la Mazingira (NEMC, Manispaa ya Kinondoni pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumnba na Maendeleo ya Makazi kutokana na mmiliki huyo kushindwa kubomoa mwenyewe kwa maelekezo ya aliyopewa na Serikali.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo la kubomoa uzio huo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema kuwa maeneo yote ya Ufukwe wa Bahari ni maeneo ya jamii hivyo hayatakiwi kuguswa kwa namna yeyote ile.
Waziri Lukuvi amesema serikali haitakubali kuona maeneo yanavamiwa na watu wachache kwa kuzunguka baadhi ya watendaji na kupata hati.
Amesema kuwa katika kipindi hiki watafatilia maeneo yote ya ardhi kama yamevamiwa na yatarudishwa kwa ajili ya maendeleo ya jamii

Hakuna maoni
Chapisha Maoni