Zinazobamba

JUKWAA LA WAHARIRI NCHINI WAPATA SAFU YAKE MPYA YA UONGOZI,SOMA HAPO KUJUA

Mkurugenzi wa Kampuni ya Uhuru Publisher, Theophil Makunga
Mkurugenzi wa Kampuni ya Uhuru Publisher, Theophil Makunga

THEOPHIL Makunga ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Uhuru Publisher, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF). Anaandika Yusuph Katimba … (endelea).
Katika mkutano wa kuchagua mwenyekiti mpya wa jukwaa hilo baada ya aliyekuwa mwenyekiti wake Absalom Kibanda kumaliza muda wake, Makunga alipata kura 34 dhidi ya mpinzani wake Joseph Kwayu ambaye ni Mhariri Mkuu wa gazeti la Guardian kupata kura 32.
Uchaguzi huo umefanyika leo Mjini Morogoro katika Hoteli ya Nashera.
Uchaguzi huo umehusisha nafasi nne za uongozi ambapo Deodatus Balile wa Gazeti la Jamhuri amekuwa makamu mwenyekiti wa TEF kwa kupata kura 47 huku Bakari Machumu ambaye ni mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi akipata kura 17.
Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Nevile Meena ameendelea kuwa katibu wa jukwaa huku msaidizi Nengida Johanes kutoka Radio na gazeti Upendo.

Hakuna maoni