MKE WA DAVID KAFULILA ALIKOMALIA SAKATA LA ESCROW BUNGENI,SOMA HAPO KUJUA
Mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Jesca Kishoa, amehoji kwa nini Tasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru), imesema watu 36 watafikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi lakini vinara wa kashfa ya Tegeta Escrow, ikiwa ni pamoja na Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Habirnder Seth Singh, hayumo.
Kishowa ni mke wa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye aliishupalia hoja hiyo bungeni na kuwang’oa baadhi ya vigogo wa serikali wakiwemo mawaziri.
Kafulila ndiye Mbunge wa kwanza kuifikisha kashfa hiyo kwenye Bungeni la 10 na baadaye Ofisi ya Mdhimiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ikafanya uchunguzi na kuwasilisha ripoti yake ambayo ilifikishwa Bungeni na Kamati ya Hesabu za Serikali.
Kashfa hiyo ilisababisha aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kuachia ngazi.
Watumishi wengine walioguswa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, Wenyeviti wa Kamati ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa, Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, William Ngeleja na Kamati ya Bajeti, Andrew Chenge.
Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, alikumbwa na fagio hilo.
Kwenye mkutano wa jana wa Bunge, Kishowa alitaka kupewa maelezo kwa nini mmliki huyo wa IPTL hajachukuliwa hatua na kusema hata baadhi ya maazimio ya Bunge yaliyopitishwa hayajafanyiwa kazi.
Alisema ingawa anajua Mwenyekiti aliyekuwa akiongoza kikao cha jana, Chenge, ana maslahi katika suala hilo ni vyema akatoa mwongozo wa kiti.
Akijibu mwongozo huo, Chenge alisema, limeulizwa sehemu ambapo siyo kabisa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni