SAKATA LA SERIKALI YA MAGUFULI KUMWONDOLEA MLINZI LOWASSA,CHADEMA NAYO YAJIPANGA,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
WAKATI kukiwa bado kuna sinto fahamu juu ya
kuondolewa kwa Alocye Tendewa ambaye ni Mlinzi wa Aliyekuwa mgombea wa Urais
kupitia chama cha deomrasia na maendeleo Chadema,Edward lowassa, baada ya
mlinzi huyo kurejeshwa serikalini,
Nacho chama cha Chadema kipo mbioni kumwandalia Lowassa mlinzi
atakayeendelea kumlinda na kumweka salama.
Taarifa za kuondolewa Mlinzi mmoja wa Lowassa na
kuachiwa mlinzi mmoja anayeitwa Samson
Machaba zilitolewa jana na ofisi ya Lowassa,
Ambapo inaelezwa kuwa mawaziri wakuu wakishastaafu anatakiwa kupewa
walinzi wawili ambao wanamlinda siku zote atakazokuwa duniani,ambao Tendewa
alimlinda lowassa takribani miaka kumi lakini,taarifa za hivi karibuni zinadai kuwa
mlinzi huyo amemuliwa na mwajili wake ambaye ni serikali arudi ofisi ya waziri
mkuu.
Lowassa
ambaye alikuwa waziri wa awamu ya nne ambapo alidumu kwenye nafasi yake kwa
kipindi cha miaka miwili ndipo baade alijiuzulu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika kilichopo
ndani ya Chadema kimeumbia mtandao huu kuwa chadema kimepokea kwa mshtuko hatua
ya serikali kumwondolea mlinzi mmoja lowassa wakati kisheria anatakiwa kuwa na
walinzi wawili.
“Yaani hata sisi tumeshangaa,maana mawaziri wakuu wanatakiwa
kuwa na walinzi tena,wanakulinda katika vipindi vyote,ila tunashangaa leo
kwanini serikali imeamua kumwondoa mlinzi Yule harafu bila hata kutoa taarifa
ni kwanini wanampunguzia mlinzi”kimesema chanzo chetu hicho.
Mtoa taarifa huyo amezidi uambia mtandao kuwa chadema
inasubiri taarifa kutoka kwa lowassa kuona ni
kama serikali itaendelea kumnyima lowassa mlinzi basi Chadema watafanya
utaratibu wakumpatia ulinzi,
“Sikufichi chadema ni chama makini na kinawalinda
viongozi wake kwa fedha yeyote ile,ninachokwambia kama serikali haitokuja na
jibu kuhusu hatma ya Waziri mkuu mstaafu Lowassa,basi chama chetu kinawalinzi
ambao wamebobea tunampa mlinzi tu,kwa sasa tunangojea serikali itasemaje”
Kuondolewa huko Mlinzi lowassa kunazidi kwenda
tofauti na mawaziri wakuu wote ambao waliongoza kwani Fredrick Sumaye,Mizengo
Pinda,na wengine ambao wote wanawalinzi wawili ambao wanawalinda lakini swali
linazidi ibua hisia ni kwanini lowassa aondolewe ulinzi.
Maoni 1
Aloyce Tendewa ninaamini ni mmoja kati ya walinzi BORA sana kupata kutokea ktk medani ya ulinzi. Ninakiri kuwa ni mtu makini sana awapo ndani ya kazi na hata nje ya kazi. Ikumbukwe kuwa watu wa aina yake kwa sasa ni nadra sana kuwapata ktk IDARA. Kwa aina ya utendaji wake na kwa HITAJI la huduma yake kwa sasa na haswa wakati huu, nadani huenda ikawa amepangiwa JUKUMU jingine ZITO ambalo lina TIJA kwa TAIFA. Hivyo nina uhakika serikali itamtafuta mbadala wake na ataendelea kutekeleza majukumu yake ya ulinzi kwa Mh Edward Lowassa kama ilivyo taratibu AGIZWA. Ninaamini ni mabadiliko ya kawaida ya kikazi yenye lengo la kuleta TIJA na sii kama ambavyo linavyo chukuliwa kwa fikra HASI kama ilivyo sasa. Mh Lowassa bado ni kiongozi wa kitaifa anaye stahili stahiki zote za kitaifa ikiwa ni pamoja na ULINZI WAKE na familia yake.
Chapisha Maoni