Zinazobamba

37 MBARONI KWA KUTOA VITISHO NA MATUSI MAZITO MTANDAONI.


Na Mwandishi Wetu.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Aprili 20 mwaka huu katika eneo la Ubungo Dar es Salaam limewakamata watu 37 kwa tuhuma za makosa ya kimtandao ikiwemo kutoa vitisho na lugha za matusi mazito kwa watu mbalimbali.

Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 27,2026 na Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam SACP Jumanne Muliro wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam.


SACP Muliro amebainisha kuwa kundi hilo baadhi yao wamebainika ni wafanyakazi wa kampuni ya INNOVIX CALL CO LTD na OTAIGO FINANCIAL SERVICES COMPANY LIMITED inayojishughulisha na ukopeshaji wa pesa kwa njia ya mtandao.


Aidha amewataja  watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Renatus Mujwahuzi Migeyo mkazi wa Mbezi Beach,Odilia Oswin Ngunga mkazi wa Goba njia nne,Theresia Brastius Kanu mkazi wa Mtoni Kijichi na wenzao 34.


"Hatua zaidi zinachukuliwa ili kuwafikisha kwenye mamlaka zingine za kisheria"amesema SACP Muliro.


Vilevile ameongeza kuwa katika kutekeleza na kusimamia mifumo ya haki jinai Polisi Dar es Salaam

kwa mara nyingine inawashukuru wananchi na wadau wengine wa usalama kwa kuendelea kuwashughulikia watuhumiwa wa vitendo vya kijinai kwa

kutumia mifumo ya kisheria. 


Amesema kuwa Polisi Dar es Salaam ina baadhi ya takwimu za kipindi cha mwezi Machi hadi Aprili 2026 ambazo baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa na kufukishwa kwenye mifumo mingine ya kisheria

1walipatikana na hatia.


"Watuhumiwa waliopatikana na hatia ni pamoja,Hashimu Kasimu Duma mkazi wa Kimara alihukumiwa na Mahakama ya

Wilaya ya Ubungo kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti,pia Vicent Laurent Ndimbo mkazi wa Urafiki Kinondoni alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka,


Habibu Nassoro mkazi Charambe alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Temeke kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti,Ismail Ally Muro Mkazi wa

Charambe alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Temeke kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka.


Wengine ni Nelson Julius mkazi wa Mavurunza

Kimara alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Ubungo kifungo cha miaka

30 jela kwa kosa la unyang ‘anyi wa kutumia silaha,Fadhili Issa mkazi wa Mbagala alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Temeke kifungo cha

miaka 30 jela kwa kosa la kubaka,


Peniel Jonathan Mtakibaleza mkazi

wa Mbagala alihukumiwa na Mahakama ya Temeke kifungo cha miaka 30

jela kwa kosa la kubaka,Yusuph Iddi mkazi wa Mbagala alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Temeke kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la

kubaka na kumpa mimba mwanafunzi.


Hata hivyo Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa mbalimbali

zenye viashiria vya kihalifu ili ziweze kufanyiwa kazi kwa haraka na kwenda mahakamani kutoa ushahidi ili haki iweze kutendeka na kuonekana.


No comments