PROFESA LIPUMBA AIBUKA TENA OFISI ZA CUF,SASA AMVAA RAIS SHEIN,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
ALIYEKUWA mwenyekiti wa Chama cha
Wananchi,CUF,Profesa Ibrahim Lipumba amemtaka Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Dkt Mohamed Shein kuacha kung’ang’ania madaraka, badala yake amemtaka
kumwachia mgombea wa Urais wa CUF Maalim seif shaarif Hamad ambaye amedai ni mshindi
halari,
Hata hivyo,
amesema Dkt Shein akiendelea kukaidi
basi atapelekea kutokea machafuko makubwa ambayo yaliwai kutokea visiwani
Zanzibar mwaka 2001.
Profesa
Lipumba ambaye alijiuuzulu nafasi ya Uenyekiti wa CUF miezi mitano iliyopita
kutokana na kutokubaliana aliyekuwa
Mgombea wa Urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,Edward
Lowassa ambaye chama cha CUF kilikuwa kinamuunga mkono,
Ambapo
Leo Profesa Lipumba ameibuka tena kwenye Makao mkuu ya CUF yalioko Buguruni Jijini
Dar es salaam na kuzungumza na waandishi wa habari ambapo Amesema Dkt Shein
anatakiwa kuachia madaraka kwa madai kuwa ameshindwa kwenye uchaguzi mkuu
uliomalizika.
‘Mimi namsihi Dkta shein aache ukaidi,ameshashindwa
kwenye uchaguzi ule,akubali Mgombea wa CUF ambaye ameshinda kihalari aongoze
maana anavyozidi kuendelea kung’ang’ania ataweza hata kuharibu amani na utulivu
ulioko visiwani zanzibar na kuingiza Zanzibar kwenye machafuku kama ya mwaka
2001”amesema Profesa Lipumba.
Amesema
kuwa kitendo cha Dtk Shein kuendelea kubaki madarakani na kung’ang’ania
uchaguzi urudiwe akikubaliki amedai kuwa kunazidi ichafua Jamhuri ya Mungano wa
Tanzania kwenye medani ya kimataifa.
Ameeleza
kuwa hatua iliyochukuliwa shirika la
Millennium Challenge Corporatinon-MCC kwa serikali ya Tanzania kuinyimwa msaada
wa dola Milioni 698,kutokana na kile anachokiita ni “Ubabe” wa Dkt Shein kubaki
madarakani kunazidi dharotesha uchumi wa Tanzania.
“Dkt Shein anachofanya cha kutokubali matokeo ya
uchaguzi wa Zanzibar kutaathiri mahusiano yetu na nchi nyengine hasa jumuiya za
ulaya,ajiuulize suala la msingi anataka kuleta machafuko ya kisiasa
Zanzibar”ameongeza
Profesa Lipumba ambaye ni msomi wa uchumi amefafanua
hasara ya kiuchumi ambazo Taifa litaweza kuzipata kutokana na mgogoro huo,kwa
kudai kuwa Tanzania itafutwa kwenye mpango wa Rais wa Marekani
Barack Obama wa kuisadia nchi katika kupata umeme katika kila vijiji,
“Huyu Shein anataka kumuhujumu Rais Obama
asifanikishe mpango bwake wa power Afrika kabla hajang’atuka mwaka 2016?,alihoji
Profesa Lipumba
Pamoja na hayo,Profesa Lipumba amemuomba Rais John
Magufuli kuitaka tume ya uchaguzi Zanzibar,ZEC
kutangaza matokeo yaliyobaki ili nchi iweze kusonga mbele,
Hakuna maoni
Chapisha Maoni