DC MAKONDA APANIA KUMALIZA TATIZO LA UHABA WA SHULE ZA SEKONDARI,SOMA HAPO KUJUA
![]() | ||
Pichani ni mkuu wa wilaya ya Kinondoni,Paul Makonda |
KATIKA kukabiliana na tatizo la ukosefu wa shule za
Sekondali za kata katika manispaa ya
Kinondoni,mkuu wa wilaya hiyo,Paul Makonda amesema amedhamilia kujenga shule
hizo sita kuanzia Januari 5 hapo mwakani.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Makonda
ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa
habari ambapo ameeleza kuwa wilaya yake inatatizo la ukosefu wa shule hizo
jambo analodai limechangia wanafunzi wengi kukosa nafasi ya kujiinga na kidato
cha kwanza kutokana na ukosefu wa shule hizo,
Ametole mfano matokeo ya darasa la saba ya mwaka
huu
yanaonyesha wanafunzi 15,185 walipata nafasi ya kujiiunga na shule za sekondari
katika chaguo la kwanza lakini kati ya
wanafunzi hao wanafunzi 3,183 licha kufahulu kwao wamekosa nafasi ya kujiiunga
na kidato cha kwanza kutokana na ukosefu wa shule,
Makonda
ameyataja maeneo yaliokumbana na uhaba wa shule hizi ni katika kata za
Mzimuni,Ubungu,Kimara,Kinondoni,Magomeni na Mbezi juu,
Amesema
baada ya kubaini shida hizo amechukua hatua ikiwemo kushirikiana na wadau wa
maendeleo walioko ndani ya wilaya yake hiyo kuhakikisha wanapata fedha za
kuhakikisha wanaanza ujenzi wa shule hizo haraka sana.
Ameongeza
kuwa Ujenzi wa shule hizo utakwenda na kasi ya haraka ikiwemo kufanya kazi
usiku na mchana katika ujenzi wake ili
kuhakikisha wanafunzi hao waliokosa kujiiunga kidato cha kwanza
wanajiiunga haraka na kuanza masomo yao.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni