VURUGU ZA DAR LEO KUHUSU BOMOA BOMOA,KOVA AWAJIA JUU WANANCHI ,SOMA HAPO KUJUA

NA KAROLI VINSENT
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam
limewataka wananchi wa maeneo ambayo baraza la Mazingira,NEMC linapita likiweka
alama ya ‘ X’ kwa ajili ya kubomolewa kuacha kuwafanyia fujo maofisa hao, lasivyo jeshi
halitasita kumchukulia hatua kali mtu au watu watakao washambulia watendaji hao
wa Nemc.
Kalipio hilo la jeshi la polisi linakuja ikiwa ni
saa chache kupita baada ya wakazi wa maeneo ya Jangwani,Kigogo Jijini Dar es
Salaam kujitokeza na kufunga barabara zote zipitazo maeneo hayo kwa kile
wanachokidai kuwazuia maafisa wa NEMC wanaoweka alama ya X kwa ajili ya
kuwakumbusha wakazi hao kujiiandaa kuhama kabla ya wiki ijiyo bomoabomoa inatarajia kuaanza.
Akizungumza na waandishi wa habari jioni hii ya leo
Jijini Dar es Salaam,Kamishna wa Kanda Maalum,Suleiman Kova amesema Jeshi hilo
limepokea kwa masikitiko kwa wananchi ambao ni wavunjaji wa sheria wanaowavamia
maofisa wa NEMC kuwazuia kufanya kazi zao.
“Tumepata taarifa hizo,tukawatuma maaskari wameenda
pale wamefanikiwa kuzuia fujo hizo,ila nawaambia wananchi waheshim sheria za
nchi na utawala uliopo madarakani,nawahakikishia kuwa tutaweka ulinzi hadi siku
ya kuanza kuzibomoa nyumba hizo siku jumanne”amesema Kova.
Kova ameongeza kuwa kwa sasa ni lazima nyumba hizo
zivunjwe kwani zimekiuka sheria ya ardhi,mazingira pamoja na mipango miji jambo
analodai kuwa serikali hii itazivunja bila hata kumwogopa mtu.
Alipohitajika kuzungumzia zoezi
hilo kwakuwa alikuwepo wakati tukio zima hadi kumalizika kwakwe, Heche aligoma
kuzungumzia zoezi hilo kwa kudai kuwa mzungumzaji mkuu ni Waziri anayehusika na
Mazingira, January Makamba au Mkurugenzi wa NEMC.
Miongoni mwa malalamiko ya wananchi waishio katika bonde hilo ni kutaka jengo la Stendi ya mabasi yaendayo haraka pia liwekewe alama na hatimaye kubomolewa kwa sababu ya kuwa jengo hilo lipo bondeni sawa na nyumba zao,
Aidha wameiomba serikali kuongeza siku zaidi za maandalizi ili waweze kuhamisha vitu vya majumbani kwani muda uliotolewa hautoshi kufanya maandalizi.
Ikumbukwe kuwa zoezi la kubomoa nyumba zilizopo mabondeni lilianza Desemba 17 mwaka huu na kusitishwa baada ya siku tatu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi hadi Januari 5 kwa kigezo cha kutoa nafasi kwa watu waliojenga katika maeneo hayo kuondoa wenyewe mali zao .

Hakuna maoni
Chapisha Maoni