RUNGU LA MAGUFULI KUZIANGUKIA BAA,MAKANISA,VIWANDA,SASA KUFUNGWA RASMI,NEMC YASEMA KANUNI IMESHAPATIKANA,SOMA HAPO KUJUA
BARAZA la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) limesema
litazifunga Baa,Makanisa pamoja na Viwanda ambavyo vimekuwa vingifungilia sauti
kubwa ambazo zinawakela wananchi.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hatua hiyo imetangazwa leo Jijini Dar es Salaam na
Mkurugenzi wa NEMC mhandisi Bonaventure Baya wakati akizungumza na waandishi wa
habari ambapo amesema mara baada ya sheria ya mazingira ya mwaka 2004
kupatikana kanuni zake ambazo kanuni hizo zinaruhusu rasmi kutimika kwa sheria
hiyo,
Amesema sheria hiyo ya mwaka 2004 imetoa katazo
kwa mtu yeyote kusababisha kelele yenye
kubughuzi,kudhuru,kuhatarisha faraja ya mtu mwengine.
Hata hivyo sheria hiyo imeweka adhabu kwa mtu
atakayekaidi sheria hiyo na kuendelea na kupiga kelele kwa wananchi kwa kuanisha
adhabu kwa mahakama isiyopungua Tshas 50,000 na isiyozidi milioni 50,
Sanjari na faini hizo pia kanuni hiyo ya mazingira kifungo 194 (1) inatoa mamlaka
kwa NEMC ku
fungia eneo au kuweka katazo kwa sehemu husika ambayo imekubuhu kwa
kelele hizo,
Baya ameyataja maeneo ambayo yamekuwa yakilalamikiwana
wananchi kukidhili kwa kelele ni Viwandani,baadhi ya makanisa,pamoja na
viwandani,
Vilevile Baraza hilo limesema litahakikisha
linashirikiana na sekta zote,wizara.Mamlaka za Serikali za miotaa na
Halmashauri na Manispaa ya majiji pamoja na mamlaka zote za umma kwa ujumla
lili kuzingatia na kuetekeleza kanuni hizo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni