MASIKINI MBUNGE MTEMVU WA JIMBO LA TEMEKE,AZOMEWA JUKWAANI MPAKA AKIMBIA,NI MATOKEO YA NGUVU YA UMMA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani wakati kati ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Temeke,Abbas Mtevu, |
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Temeke kwa tiketi ya
Chama cha Mapinduzi CCM,Abbas mtemvu imemlazikia kushuka kwenye jukwaa alilokuwa
akilitumia kunadi sera,baada ya umati mkubwa wa vijana kumzomea pamoja na
kumrushia chupa za maji.Anaadika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Tukio hilo
la aina yake limetokea Leo Majira ya asubuhi kwenye viwanja vya mwembe Yanga
wakati Mgombea huyo alipokuwa anawatubia Vijana wa “joking” kutoka maeneo mbali
mbali ya Temeke jijini Dar es Salaa
wakati alikuwa akiwaomba wamchagua tena kuwa Mbunge katika Jimbo hilo.
Mtemvu
licha ya mkutano wake huo kusindikizwa na wasanii wanaotamba kwa miziki ya
uswahilini inayojulikana kama “vigodoro”
wasanii hao ni Dogo Diga pamoja na Dj
Man fongo ambao wote kwa pamoja walikuwa ni wa kwanza kupanda katika jukwaa wakiimba
huku wakishangiliwa na vijana mbali mbali waliokuwepo Uwanjani hapo,
Mara
baada ya kumaliza kuimba wasanii hao wa "visingeli",ndipo ikafika wakati wa Mtevu
kupanda Jukwaani na kuwaeleza nia ya yeye kutaka kuendelea kugombani Ubunge kwa
awamu nyingine ya Nne katika jimbo,
Ndipo
aliposhika kipaza sauti akianza kujinadi, huku akisema “CCM oyee” jambo
liliwachukiza watu waliokuwepo uwanjani hapo, ndipo nao wakaanza kutoa ishara
inayotumiwa na mgombea Urais kupitia Chadema ,Edward lowassa ambaye anaungwa
mkono na Vyama vya Ukawa, yakuzungurusha mikono huku wakiimba kwa pamoja “Lowassa
mabadiliko,mabadiliko Lowassa”huku wakimzomea Mbunge huyo,
Jambo
lilomfanya Mtevu kushindwa hata kuzungumza na ikamlazimua kushuka jukwaani hapo
na kuondoka Uwanjani hapo kuebuka Vurugu,
WANANCHI WA
TEMEKE WA NENA.
Wakizungumza kwa wakati mmoja na fullhabari.blog,wananchi wa jimbo la
Temeke waliokuwa uwanjani hapo wamesema,Hawamtaki mgombea huyo wa CCM kwani
katika kipindi cha miaka 15 alichokuwa mbunge hakuna alichokifanya kwenye
jImbo hilo.
“Huyu
bwana amekaa zadi ya mika 15 hakuna alichofanya amekuwa Mbunge wa kulala
Bungeni huku akishindwa hata kutusaidia sisi wakazi wa Jimboni kwake,tumemchoka
bora aondoke kabisa na leo hii ni trela muvi kamili ataiyona octoba 25
hatuitaki CCM tena”Amesema ally Said mkazi wa Temeke.
Mbali na huyo
Mkazi, mwengineni Mama Juma naye pia alimtupia lawama Mbunge huyo kwa kusema
miaka yote aliyokuwa Mbunge wa Jimbo la Dar es Salaam,ameshindwa kuoka wizi unaofanywa
na Mameya wa jiji.
“Yaani amekuwa mbunge,miongoni mwa majimbo ya Dar es
Salaam,amehusika kwa maksudi katika kunyamazia uuzwaji wa bei ya kutupwa,shirika
la usafirishaji wa Uda,kwa familiya ya vigogo wa Ikulu,leo anakuja kutulilia
sisi,kwa taarifa yake ndio hajue kwamba hatumtaki”amesema mama huyo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni