Zinazobamba

LOWASSA AMCHANGANYA JANUARY MAKAMBA,SASA ALIA NA MAGAZETI KUHUSU LOWASSA,SOMA HAPO KUJUA

NA KAROLI VINSENT
WAKATI  chama cha Mapinduzi CCM kikituhumiwa kuyatumia Magazeti ya Uhuru,Tazama,Dira Mtanzania,Mikakati pamoja na Raia Tanzania kuripoti habari za kiplopaganda na za kizushi kwa Mgombea wa Urais kupitia Chadema Edward Lowassa,
     Sasa CCM ni kama kimeanza kuweweseka na kusema Magazeti nchini yanampendelea Lowassa,
        Hayo yamesemwa na  Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, January Makamba ameonesha kutokubaliana kwake na ripoti za kinachojili kwenye mikutano ya mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa na kueleza kuwa  Magazeti hutumiwa kupiga kampeni.

Makamba ameeleza hayo kupitia mtandao wa Twitter baada ya mtu mmoja anaetumia jina la ‘Gachanja Muigai’, kumueleza kuwa kutokana na kile wananachokisoma, inaonekana kuwa wananchi wengi wanamuunga mkono Lowassa. Na akataka kupata maoni ya Makamba kutokana na hali hiyo kama anadhani wataweza kushinda.

 @JMakamba @MagufuliJP From what we read here, it seems #Lowassa is resonating with Wananchi. Una hakika si wakati wa kuvuka sakafu?” Aliuliza.
Makamba alimjibu kuwa wapinzani wanatumia baadhi ya magazeti kama sehemu ya kampeni zao lakini tafiti na hali halisi nchini inaeleza tofauti.
“They’ve turned some newspapers into their campaign fliers. But the polls & mood across Tanzania tell another story.”
Mpekuzi blog

Maoni 1

Bila jina alisema ...

januari makamba kwa maana nyingine anatangaza uhasama wa kujitakia baina ya waandishi wengi wa habari ndani na nje ya nchi na chama chake-ccm- anawashambulia kwa sababu tuu hawairembi na kuipendelea ccm.kazi ya uandishi ni kazi ya dhamana na heshima kubwa kwa jamii.siku zote jamii inawategemea waandishi wawahabarishe,habari za kweli na si vinginevyo.waandishi wanasafiri,wanahoji,wanasikia na,wanapaswa-kwa haki na ukweli-kuanndika uhalisia wa matukio,na,ndivyo wanavyofanya.kwa hali hiyo januari na chama-dola ccm wananchi wako upande wa lowasa na wajue kwa sasa wajiandae tuu mnamo novemba kukaa upande wa pili wa bunge letu kama chama kipya cha upinzani.muda wao umewadia,hakuna jinsi.