HABARI NJEMA JIJINI DAR,FLAY OVER UJENZI WAKE KUANZA MWEZI UJAO,SOMA HAPO KUJUA
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi5cbC2QoBaG8EMGXjTyuDU3iQ3cy91_sHb1D4yeOSriAGMI8Bf4bKTpG7bj1efl2zsMhCL2Z8s8QwVx0-WKqgNPQXwbn4Vw4FflWOdb8cjhhc1He41bBNOxl94WwymfpeOBamznMisFL9l/s640/9.jpg)
SERIKALI imesema Ujenzi wa Flay Over kwenye Makutano
ya Barabarabra ya Tazara jijini Dar es Salaam yanatarajia kuanza mapema mwezi
ujao,Anaandika KAROLI VISENT endelea nayo.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa
Ujenzi DK John Magufuli wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa Habari
ambapo amesema baada ya hatua zote za mradi wa ujenzi wa Fray over hiyo
kukamilika sasa kinachofuata ni Mkandarasi wa Kampuni ya Oriental Consultant
ltd kutoka Japani kuanza kazi hiyo,
Magufuli amesema Mradi huo ambao utagalimu jumla ya
pesa za kitanzania Bilioni 87.156 pesa hizo ambazo ni za msaada kutoka Serikali ya Japani,unatarajia kumalizika baada
ya miezi 32 kutoka sasa,
Ameongeza
kuwa mradi huo utakuwa na awamu mbili hawamu ya kwanza itachukua miezi 12 ya upembezzi na miezi itakayobakia ni kukamilisha
ujenzi wa Fyay over,
Magufuli
ambaye pia ni mgombea wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM amesema
kukamilika kwa Fya over hiyo kutasaidia kupunguza msongamano wa Magari Jijini
Dar es salaam,
Hakuna maoni
Chapisha Maoni