GOLI LA MKONO LADAKWA,INATISHA NEC YAFANYA UTAPELI WA KUTISHA,CHADEMA YABAINI DAFTARI HEWA,SOMA HAPO KUJUA
Mwanasheria kutoka CHADEMA Bwana JOHN MALLYA akionyesha baadhi ya vifungu vya sheria ambavyo vinaruhusu wapiga kura kukaa meter mia mbili kulinda kura zao |
Katika hali ya kushangaza baada ya Tume ta uchaguzi kusambaza nakala ya daftari la kudumu la wapiga kura kwa vyama vya siasa jana jioni hatimaye madudu makubwa yameanza kubainika ndani ya daftari hilo jambo lililozua taharuki kubwa kwa vyama kadhaa huku wakiwa hawana imani na daftari hilo tena.
Picha za wapiga kura kutoka kituo cha Dodoma Mjini ambazo zipo kmwenye daftari la kudumu la wapiga kura lililotolewa na Tume hiyo Huku picha nyingine zikiwa hazina wahusika zikiwa na giza na majengo |
Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA wamekuwa wa kwanza kujitokeza mbele ya wanahabari baada ya kuanza kulikagua daftari hilo na kuonyesha madudu makubwa ambayo wamedai yanafanyika na tume hiyo kwa ajili ya kukisaidia chama tawala kiweze kuendelea kuwa madarakani.
Akizungumza na wanahabari mchana wa leo Mkurugenzi wa uchaguzi kutoka chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA Bwana REGNAD MUNISHI ameeleza mambo ambayo yamejitokeza ndani ya daftari hilo ambayo ni ya kushangaza ikiwemo kuwepo kwa picha ambazo hazina sura za watu zikiwa na giza,kuwepo kwa picha za majengo ambazo zimepewa vitambulisho,Picha za watu wawili kwenye Picha moja,picha za wachina,na picha ambazo hazina mandhari yanayofanana kwa kituo kimoja,jambo ambalo amedai ni utani mkubwa na hato yote ni katika kituo kimoja ndani ya Dodoma mjini nab ado wanaendelea kufanya upembuzi juu ya daftari hilo.
Mkurugenzi wa uchaguzi wa CHADEMA REGINALD MUNISHI akifafanua jambo |
Akizugumza huku akionyesha picha kadhaa ambazo zimepigwa kwenye kituo kimoja cha Dodoma Mjini MUNISHI amesema kuwa kituo kimoja kimekutwa na makosa zaidi ya 17 yote yakiwa ni ya makusudi na yanayoweza kuhatarisha uchaguzi na kuhitimisha kauli ya goli la mkoni katika uchaguzi huo.
SWALA LA KULINDA KURA.
Wakati mijadala nchini Tanzania kwa sasa ikiwa nji swala la nani anaruhusiwa kukaa karibu na vituo baada ya kupiga kura kwa kile kinachoitwa kulinda kura,umoja wa katiba ya wananchi UKAWA umeibuka na kusisitiza kuwa sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985 inamruhusu mpiga kura yoyote kukaa meter mia mbili kutoka kwenye kituo cha kupiga kura hivyo kauli za vitisho zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa chama tawala na serikali ni kauli za mfa maji na haziwezi kuwatisha katika harakati zao za kusaka mabadiliko nchini Tanzania.
Makamu Mwenyekiti CHADEMA akifafanua jambo |
Wakizungumza na wanahabari leo makamu mweyekiti wa CHADEMA Pofesa ABDALA SAFARI pamoja na mwanasheria kutoka CHADEMA Bwana JOHN MALLYA wamesema kuwa hakuna sheria inayomkataza mtanzania kulinda kura yake na kusisitiza kuwa sheria ya uchaguzi inasisitiza kuwa kukaa meter mia mbili kutoka kituo cha kupigia kura na sio vinginevyo.
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania DK JAKAYA KIKWETE akiwa sherehe za kuzima mwenge mjini Dodoma kupiga marufuku kukaa karibu na vituo vya kupigia kura huku akisema kuwa kwa atakayekiuka hilo atakumbana na nguvu kubwa ya vyombo vya dola.
Baada ya maamuzi hayo ya serikali kutangazwa jana na serikali UKAWA kupitia kwa makamu mwenyekiti nwa CHADEMA Profesa SAFARI amesema kuwa baada ya maswala hayo yanayoendelea katika uchaguzi huo wameamua kuandika barua haraka za malalamiko kwa jumuiya za kimataifa ikiwemo mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC pamoja na jumuiya za madola kulalamikia kile ambacho wanakiita rafu ya uchagfuzi inayofanywa na chama tawala ili kisitoke madarakani.
Picha moja watu wawili |
Kiongozi huyo anasema kuwa kauli ya Rais KIKWETE ya vitisho ukilinganisha na madudu ambayo yanaoneka katika daftari lililotolewa jana inaonyesha wazi kuwa kuna michazo michafu inayochezwa na seriukali ili kupingana na nguvu ya mabadiliko njambo ambalo wamesema kuwa hawatakubaliana nalo
PICHA NYINGINE ZINAENDELEA CHINI----
WAKATI Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ikiwa ndio kwanza imelikabidhi Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi, ili kufanyiwa uhakiki, uchunguzi umeonesha daftari hilo ni chafu na haliaminiki. Anaandika Charles William … (endelea).
Siri hii inafichuka siku tisa tu kabla ya Oktoba 25 ambapo Watanzania wapatao milioni 22 wanatarajiwa kujitokeza vituoni kupiga kura ya kuchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano, Wabunge na Madiwani.
Kwa Zanzibar, kutakuwa pia na uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Waakilishi na Madiwani.
Hatua hiyo inakuja siku moja tangu Tume ya Uchaguzi iruhusu vyama vya siasa kuchukua daftari hilo ndani ya shinikizo kubwa za viongozi wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Mbele ya waandishi wa habari leo, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Profesa Abdallah Safari pamoja na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa chama hicho, Reginald Munisi, walisema kumebainika “madudu na upungufu mwingi kwenye daftari. Kwa hakika haliaminiki.”
“Tumeanza kulifanyia ukaguzi daftari la Tume baada ya kulipata jana Jumatano, na kwa tuliyoyaona, sasa tumeelewa ni kwanini walikuwa hawataki kulitoa mapema,” amesema Prof. Safari ambaye ni wakili wa Mahakama Kuu nchini.
“… ni wazi Tume hii ambayo si tume huru imejiandaa kuhujumu uchaguzi kwa kuwa katika kituo kimoja tu tulichokagua tumeona majina feki mengi yakiwa yameingizwa,” ameongeza Munisi ambaye amesema ukaguzi ulifanywa katika jimbo la Dodoma mjini.
Dosari za msingi zilizobainika katika ukaguzi huo ni
- Majengo kuandikishwa kama wapiga kura. Katika hali ya kushangaza picha za majengo, ikiwemo migahawa zimeonekana kuwa ni sehemu ya majina ya wapigakura wa jimbo la Dodoma Mjini huku zikibeba majina ya watu na namba ya kitambulisho cha mpiga kura.
- Baadhi ya vitambulisho kuonekana vikiwa na picha mbili: kumekutwa baadhi ya vitambulisho vinachoandamana na picha ya halisi za watu wengine nyuma.
- Raia wa kigeni kuandikishwa: Kumekutwa majina ya wasiokuwa raia wa Tanzania wamejumuishwa kwenye daftari, majina mengine yakiwa yasiyoeleweka; picha za raia wanaoonekana kuwa wageni kama Wachina na Wazungu zimeonekana zikiwa sehemu ya wapigakura wa Tanzania; na majina yenyewe yana herufi tupu zisizo na irabu na hivyo kushindwa kusomeka. Kwa mfano limekutwa jina lililoandikwa LHPG SVWTN.
- Picha za pikipiki kutokeza kama majina ya wapigakura: kumekutwa picha za pikipiki zikiwa ni sehemu ya majina ya wapigakura huku majina na picha hizo yakiwa na namba za vitambulisho vya wapigakura.
- Majina yalioainishwa kuwa ni ya wanaume yana picha za wanawake: baadhi ya majina yalioneshwa kuwa ni ya kiume na kitambulisho kuonesha kuwa jinsia inayomiliki kitambulisho ni ya kiume lakini picha ni za wanawake.
- Picha za wapigakura kupigwa katika maeneo tofauti ikiwemo sehemu zenye mabati na mbao badala ya kitambaa kimoja kilichokuwa kikitumiwa kwenye vituo vya Tume:picha za baadhi ya wapigakura zimeonekana kwa mwonekano tofauti wa nyuma (background), ikiwemo kupigwa kwenye sehemu za mabati na mbao hivyo kuzua hofu kuwa huenda uandikishwaji uliendelea katika maeneo mengine baada ya muda wa uandikishaji kumalizika.
Prof. Safari amesema kufuatia uchafu wa daftari, wanaandaa barua kwenda jumuiya za kimataifa ili kuzitahadharisha namna ambavyo serikali ya Chama Cha Mapinduzi inavyoshirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuvuruga uchaguzi.
“Leoleo tunaandika barua na kuzituma mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, tunaipelekea pia Jumuiya ya Madola, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika pamoja na Umoja wa Mataifa kuwajulisha waone mbinu chafu za CCM kutafuta ushindi wa goli la mkono… wanajiandaa kuiingiza nchi katika machafuko,” ameeleza Prof. Safari.
Munisi amesema wanaitaka tume ya taifa ya Uchaguzi kutoa majibu juu ya daftari hilo na kulirekebisha haraka sana kabla hawajatangaza uamuzi mwingine watakaouchukua iwapo hawataridhishwa na hatua za NEC.
Maoni 1
tunawashukuru sana viongozi wa chadema kuweza kuanza kukagua kwa undani na kulikagua daftari hili muhimu la wapiga kura.wameweza kugundua matatizo ya wazi na pengine ya makusudi yanayopaswa kufafanuliwa na tume ya taifa ya uchaguzi hususani bwana kailia mkurugenzi wa tume ambaye amekua msitali wa mbele kukanusha kiila ukweli unaotolewa na ukawa -chadema.kailima amejisahau na kuwa kama vile msemaji wa chama-tawala ccm.daftari hili la mpiga kura,imeonyesha wazi sasa wapiga kura hewa wapo wengi.tunasubiri tuwasikilize ccm nao jee wanafurahia hili?
Chapisha Maoni