TAFITI :ZOEZI LA KUANDIKISHA WAPIGA KURA KWA MFUMO WA BVR HALIJAFANIKIWA TANZANIA
Mwenyekiti
wa mtandao wa Asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi nchini TACCEO Bi
MARTINA KABISAMA akifafanua jambo kwa wanahabari mapema leo
|
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC Bi HELLEN KIJO BISIMBA akifafanua jambo mbele ya wanahabari baada ya kuwasilishwa kwa report nzima ya TACCEO juu ya mchakato wa uandikishwaji wa wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo mpya wa BVR |
Imeelezwa kuwa zoezi la uandikishwajiwa wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo mpya wa kielekronic BVR limekuwa si la mafanikio kutokana na kasoro nyingi kulikumba zoezi kwa ujumla
Hayo yameibuliwa na Mtandao wa asasi za
kiraia wa kuangalia chaguzi nchini Tanzania TACCEO mapema hii leo wakati wakitoa report yao ya kitafiti kuhusu
zoezi la uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo mpya wa
kielectronic BVR lilivyoendeshwa
Akizungumza na wadau mbalimbali pamoja na wanahabari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha sheria na
haki za Binadamu Dk Hellen Kijo Bisimba amekili kuwa tafiti za TACCEO zimeonyesha kutofanikiwa kwa zoezi la uandikishwaji licha ya tume ya taifa ya uchaguzi kusisitiza kuwa zoezi hilo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa
Akizitaja kasoro moja
wapo iliyokuwa kikwazo kikubwa katika mchakato wa uandikiswaji ni kukosekana
kwa elimu mahususi ya mpiga kura juu ya zoezi la auandikishwaji na umuhimu wa
zoezi lenyewe jambo ambalo amesema kuwa limekuwa ni kikwazo kikubwa kwani wananchi
wengi walikuwa hawaelewi nini maana ya mchakato huo huku wengine wakiwa
hawataki hata kujiandikisha kwa kuhofia kuwa kuna mbinu mbalimbali zinatumika
ili kupata taarifa zao.
Amesema kuwa maeneo
mengi kulikuwa na usumbufu mkubwa wa wananchi kaumini kwa mashine zile
zilikuwa na madhara kwa afya zao,wengine wakiamini kuwa wanapimwa virusi vya
ukumwi bila kujijua huku wengine wakiamini kuwa zoezi lile ni maswala ya
kishirikina yakihusishwa pia na imani za kishetani za Fremason huku wengine
wakiamini kuwa wakiwa na vitambulisho vile vya awali haikuwa na haja ya
kujiandikisha upya, jambo ambalo amesema kuwa yote hayo ni kutokana na
kukosekana kwa elimu ya mpiga kure kipindi cha zoezi la uandikishwaji.
Chanagamaoto nyingine
ambayo TACCEO wamekiri kukutana nayo wakati wa zoezi hilo ni waandikishaji wa
zoezi hilo ikiwa na maana ya mawakala waliopewa kazi ya kuandikisha kutokuwa
na elimu ya kutosha juu ya matumizi ya mfumo huo pamoja na mashine husika jambo
ambalo wamesema kuwa lilikuwa ni changamoto kubwa kwa wafanyakazi hao na
kusababisha zoezi hilo kwenda kwa kusua sua hali ambayo wamedai ilijitokeza katika
kila eneo nchini Tanzania.
Dk Hellen Kijo Bisimba
amesema kuwa changamoto nyingine ambazo zilikuwa zikiukumba mchakato huo ni
pamoja na ubovu wa mashine ambao ulisababisha zoezi kuahirishwa mara kwa
mara,wanafunzi kukosa haki yao ya kujiandikisha,pamoja na matatizo ya kiuhakiki
ambapo watu waliokuwa hawapati nafasi ya kuhakiki taarifa zao kabla ya kupewa
kitambulisho jambo ambalo limesababisha watu wengi kupewa vitambulisho ambavyo
vina taarifa ambazo sio za kweli.
Wadau |
Akizungumza
na
wanahabari mwenyekiti wa TACCEO Bi MARTINA KABISAMA amesema kuwa ni
lazima tume ihakikishe kuwa inarekebisha kasoro zilizojitokeza katika
mchakato wa
uandikishwaji wa BVR ili usijirudie tena wakati wa uchaguzi jambo ambalo
litasaidia uchaguzi kuwa wa huru na haki kwa watanzania wote
Hakuna maoni
Chapisha Maoni