SHIRIKA LA SAVE CHILDREN LAWAKABA KOO WANASIASA KUHUSU ILANI ZAO ZA UCHAGUZI,SOMA HAPO KUJUA
SHIRIKA
lisilokuwa la serikiali linalojishughulisha na Masuala ya watoto nchini The
Save the Children limewataka wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya
vyama vya siasa kuingiza mapendekezo ya
haki za watoto katika ilani zao katika
uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktaba mwaka huu.Anaandika KAROLI VINSENT
endelea nayo.
Miongoni mwa Mapendekezo hayo ni Miundombinu ya barabarani
hususani alama za barabarani zinazohusu watoto wenye ulemavu,kwa upande wa
Elimu imetajwa pia kwenye masuala ya maji safi kwenye shule mbali mbali pamoja
malipo duni ya walimu wakitaka litazamwe,
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam
na Mwakalishi wa Bodi kuu ya ushauri
watoto kutoka Zanzibar, Suhaila Msham Mwarimwana wakati wa mkutano wa pili wa
Baraza la watoto nchini ulikuwa ukiangalia mapendekezo yao ambayo yamezingatiwa kwenye ilani mbali mbali
za vyama vya siasa.
“Mnamo Mei mwaka huu Baraza la watoto
tulikutana na viongozi mbalimbali wa
vyama vya siasa nchini ambapo tulitoa
mapendekezo yetu, na sasa tunaangalia
mapendekezo ambayo hayajaanishwa
kwenye ilani za vyama vya siasa,”amesema
Mwarimwana.
pichani ni Mwakalishi wa Bodi kuu ya ushauri watoto kutoka Zanzibar, Suhaila Msham Mwarimwana akizungumza na watoto wenzake kwenye baraza hilo |
Sanjari na hayo Baraza hilo limegusia suala la
Afya kwa kusema Dawa hakuna kwenye
Hospitari ikiwemo kukosa wahudumu wa afya kutosha pamoja na gharama kubwa za
matibabu zinatozwa wakisema mambo yanahitaji kutamwa kwa maukini na vyama vya siasa ili kuiokoa jamii kwenye matatizo
mbali mbali yanayojitokeza.
Watoto wa Baraza hilo wakiwa makini kumsikiliza mwakilishi huyu |
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Shilika
hilo,Ellen Okoedion amewataka wagombea wa uongozi kuwangalia kwa umakini suala
la watoto huku akidai nusu ya watanzania ni watoto hivyo haki zao lazima
ziheshimiwe na zilindwe
Hakuna maoni
Chapisha Maoni