MWANDISHI KUBENEA AUIBUA MZIMU WA UDA,RICHMOND,SUMAYE AMPAMBA,AWATOLEA UVIVU CCM KUHUSU CHEO,SOMA HAPO KUJUA
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea (hayupo pichani) |
SI vitisho na
matusi, wala madai ya kuwa yeye Frederick Sumaye alihama CCM na kuhamia UKAWA
kwa kutafuta cheo, vitakavyomtoa nje ya mstari wa kumuunga mkono Edward Lowassa
kuleta mabadiliko nchini. Anaandika Jabir Idrissa … (endelea).
Sumaye ambaye ni waziri mkuu mstaafu aliyetumika wakati wa serikali ya
awamu ya tatu ya Benjamin Mkapa, amesema hayo akihutubia mkutano wa uzinduzi wa
kampeni ya ubunge jimbo la Ubungo, jijini Dar es Salaam.
Sumaye,
mwanasiasa gwiji aliyekuwa waziri mkuu vipindi viwili mfululizo –Novemba
1995-2005, alishiriki uzinduzi wa kampeni akimnadi mgombea anayewakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),
Saed Kubenea.
Sumaye na Kubenea wamekuwa marafiki kiasi cha Kubenea kuongoza
mkutano wa waandishi wa habari hotelini Hyatt Kilimanjaro, Dar es Salaam, ambao
Sumaye aliutumia kutangaza nia ya kuwania uteuzi wa kugombea urais ndani ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Baada ya kukatwa
jina lake, kama alivyotendwa Lowassa, Sumaye hatimaye alihama CCM na kujiunga
na UKAWA kwa lengo la kuharakisha mabadiliko ya kuiondoa CCM madarakani.
Akihutubia
mkutano uliofanyika viwanja vya Faru vilivyoko njiapanda ya Mabibo, Sumaye
amesema hatafuti cheo kama CCM wanavyomtuhumu, kwa kuwa alikuwa waziri mkuu,
wadhifa atakaoupata tu aliyechaguliwa mbunge jimboni wakati yeye hagombei
ubunge.
Kadhalika
amesema hawezi kuwa rais kwa sababu Lowassa ndiye mgombea urais kupitia Chadema
anayewakilisha UKAWA.
“Sitafuti cheo kwa
sababu kuna cheo gani tena mimi zaidi ya urais ambao tayari tunaye mgombea Lowassa.
Waziri mkuu siwezi kuwa kwa sababu sikugombea ubunge. Nimejiunga na UKAWA
kuleta mabadiliko kwa kuiondoa CCM madarakani,” amesema.
Sumaye pia aligusia
mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi jijini Dar es Salaam, akisema amradi huo ni
wa kifisadi ambao hautapunguza msongamano kwa kuwa barabara hazitoshi.
Amempamba Kubenea akisema ni kijana mpenda haki aliyejitolea
maisha yake kupigania haki za Watanzania, hata kufikia kufungiwa gazeti lake na
serikali ya CCM kwa sababu wakiandika ukweli wa maovu ndani ya serikali.
Kubenea amesema
akiingia bungeni atapigania kurudisha kwa wananchi Shirika la Usafiri Dar es
Salaam (UDA) ambalo limeuzwa kifisadi chini ya usimamizi wa mgombea mshindani
wake Ubungo, Didas Masaburi wa CCM.
Mwandishi huyo
Hodari nchini amesema hakifanikiwa kuingia Bungeni atafichui kile anachodai ni
Ripoti Kamili ya iliyochungua Kampuni Tata ya kufua Umeme ya Richmound ambapo
amesema Ripoti iliyowasilisha Bungeni sio yenyewe.
| “nikifanikiwa
kuingia Bungeni jafahamu kule kuna kinga nitaiweka wazi ripoti Kamili kuhusu
richmound ambayo imtaja mtu aliyeiba fedha hizi,najua ripoti ziko mbili moja
anayo Mwakyembe nyingene ipo kwenye mfuko wa Samwel sitta ambayo imesema ukweli
wa sakata nzima”amesema Kubenea
Mbunge wa Ubungo,
John Mnyika alihudhuria kwa muda mfupi mkutano huo na kusema wananchi wa Ubungo
wamepata mbunge mwingine mahiri atakayewawakilisha vizuri bungeni.
Habari hii kwa hisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni