OPARESHENI FUKUZA MASABURI UBUNGO YAANZA,KUBENEA KUANZA MAPAMBANO ,SOMA HAPO KUJUA
Mgombea Urais wa tiketi ya UKAWA, Edward Lowassa (kushoto) akimnadi mgombea ubunge wa Ubungo, Saed Kubenea katika kampeni zilizofanyika Mbezi |
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Saed Kubenea atafungua rasmi pazia la kampeni zake katika
kuwania nafasi hiyo Jumapili ya tarehe 13 Septemba mwaka huu. Anaandika Pendo Omary …
(endelea).
Akizungumza na Chanzo changu Katibu
wa Kubenea, Elizabeth Mbombo amesema kampeni hizo zitazinduliwa saa 8 mchana
hadi saa 12 jioni katika viwanja vya Mpakani karibu na Mahakama ya Ndizi,
Mabibo ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye.
Sumaye alijiunga na Umoja wa Katiba
ya Wananchi (Ukawa) mwezi mmoja uliopita baada ya kile alichokiita “chama
kumekuwa kikikiuka misingi na wajibu wake kwa Watanzania.”
Mbombo anasema, “mpaka sasa kwa
kiasi kikubwa maandalizi yanaendelea vizuri. Mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu
Mstaafu, Fredrick Sumaye. Mkutano utarushwa moja kwa moja na kituo cha
televisheni cha ITV. Pia watakuwepo wasaamii mbalimbali wakiwemo Msaga sumu na
G Five.”
Elizabeth anatoa wito kwa wakazi wa
ubungo na Jiji la Dar es Slaam kuhudhuria mkutano huo na kusikiliza vipaumbele
vya mgombea uhuyo na chama chake ili kufanya maamuzi sahihi wakati wa kupiga
kura 25 Oktoba mwaka huu.
Chano;Mwanahalisi
oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni