MAGUFULI AIPONDA CCM,AISHAMBULIA SERIKALI YA KIKWETE KAMA HAKUWA WAZIRI WAKE,SOMA HAPO KUJUA
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John
Magufuli anaendelea kukosoa Serikali ya CCM inayomaliza muda wake kwa kuiacha
nchi katika dimbwi la umasikini. Anaandika
Faki Sosi …. (endelea).
Akiwa
kwenye mkutano wa kampeni Uwanja wa Mkendo, wilayani Musoma, Mkoa wa Mara,
amesema yapo mambo mengi hayapendi kwa sababu yanawaumiza wananchi na
akichaguliwa kuwa rais atayabadilisha.
Ameutaja mradi wa maji uliopangwa
kutekelezwa kupitia ziwa Victoria, aliosema kila siku unatajwa lakini
hautekelezwi huku wananchi wa Mkoa wa Mara wakiendelea kupata shida ya maji.
Amesema haina maana kuwa na Waziri wa
Maji wakati kunakuwa na mradi usiokwisha, akiwahakikishia wananchi kuwa
atakapokuwa Rais, hawezi kushindwa kupata Sh. Bilioni 44 za kutekeleza mradi
huo.
Dk. Magufuli ambaye amekuwa waziri
katika serikali ya CCM kwa muda mrefu tangu alipoteuliwa kwa mara ya kwanza
naibu waziri wa ujenzi mwaka 1995.
Kufufua viwanda vilivyo uliwa na watu
kwa makusudi ambako kulikuwa na viwanda vingi ambavyo vimekufa mikononi mwa
serikali ya CCM
“Naombeni kura zenu wananchi wa Musoma
ili tuwatoe watu waovu kwani Serikali haitoki, watatoka watu wabaya ambao
nitawatoa haraka sana,” amesema.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni