MWANDISHI KUBENEA KUMVAA DK SLAA,KUTOA KILA KITU USICHOKIJUA,ASEMA AOGOPI MTU,SOMA HAPO KUJUA
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa |
NIMEMSIKILIZA kwa makini, Dk. Willibroad Slaa, aliyekuwa katibu
mkuu wa Chadema na mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Anaandika Saed Kubenea … (endelea).
Akihojiwa
na kituo cha televisheni cha Star TV, Dk. Slaa alimtuhumu Edward Lowassa kuwa
ni fisadi na akataka wananchi kumchagua “mgombea mwenye nafuu ya ufisadi.”
Akamtaja John Pombe Magufuli.
Ameeleza pia kuwa taarifa mpya
aliyonayo na ambayo aliitumia katika mkutano wake na waandishi wa habari
Jumanne iliyopita, kuhusu sakata la Richmond, aliipata kutoka kwa Dk. Harrison
Mwakyembe, aliyekuwa mwenyekiti wa kamati Teule ya Bunge, juu ya Richmond.
Niliamua kutojibizana na Dk. Slaa –
rafiki yangu wa miaka mingi – katika mradi wake huu. Lakini kwa hapa alipofika,
uvumivu umenishinda. Sitaruhusu mtu mzima, anayejiita padri na ambaye alitaka
kuwa rais wetu, kuendelea
kulindanganya taifa na kuwapotosha wananchi.
Hivyo basi, nimeamua kuanzia
leo hii, kukabiliana na Dk. Slaa kwa kila kona ili ukweli ufahamike. Kwa
kuanzia, leo hii – Jumamosi, naelekea mkoani Mbeya ambako nitahutubia wananchi
katika mkutano wa hadhara katika jimbo la Kyera, linaloshikiliwa na Mwakyembe,
swahiba mpya wa Dk. Slaa.
Nikiwa Mbeya nitaeleza ukweli
wa kilichotokea na kile ambacho Dk. Slaa anakificha.
Aidha, nikirejea Dar es
Salaam, nimepanga kuitisha mkutano na waandishi wa habari, kueleza ukweli
uliokamilika kuhusu Dk. Slaa na mkewe Josephine Mushumbuzi na sababu ya yeye
kususia chama.
ENDELEA KUFUATILIA FULLHABARI.BLOG UTAPATA MAJIBU YA KUBENEA KWA SLAA IKIWEMO KUFICHUA NYUMA YA PAAZIA USIYOYAJUA YA DOKTA SLAA
Hakuna maoni
Chapisha Maoni