OPARESHENI ONDOA MBUNGE ZUNGU ILALA YAANZA,KAMANDA HASSANALI AANZA VITA KUBWA,SOMA HAPO KUJUA
Mgombea Ubunge katika Jimbo la Ilala kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Muslim Hassanali (katikati) |
MGOMBEA Ubunge katika Jimbo la Ilala kwa tiketi ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Muslim Hassanali amezindua rasmi kampeni
zake katika jimbo hilo la mkoani Dar es Salaam. Anaandika Sarafina Lidwino …
(endelea).
Hassanali ambae pia amepania
kuziangusha ngome za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kumuondoa mbunge
aliyejichimbia kwa vipindi viwili, Mussa Zungu, katika uchaguzi mkuu ujao, kwa
kuwapatia wananchi wa Ilala maendeleo wenye kiu nayo.
Hassanali ambaye amezindua kampeni
zake leo kwenye viwanja vya Karume Sokoni amewaahidi wakazi wa jmbo kuwa tayari
kwa ajili ya kupokea mabadiliko kutoka katika muungano unaoundwa na vyama vinne
– Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
UKAWA unaundwa na Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Chama Cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na National
League for Democracy (NLD), ambapo amesema kwa kupitia muungano huwa viongozi
wa chini watakuwa na nguvu ya kuleta maendeleo.
Akizungumza na waandishi wa habari
kabla ya kupanda jukwaani kuwahutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi
kumsikiliza katika viwanja hivyo Hassanali amesema muda wa mabadiliko kwa
wakazi wa Ilala ni sasa hivyo CCM ijiandae kung’oka madarakani.
“Mmewapa CCM dola kwa miaka 54 sasa
walichokifanya hamna miaka yote hiyo, ni zamu yetu wananchi naombeni mtupe sisi
dola mwaka huu na kuahidi ndani ya miaka mitano tu mtaona mabadilko. Watanzania
wasubiri neema mwaka huu,” amesema Hassanali.
Amesema umuhimu wa kuiondoa CCM
unakuja kwa kuwa chama hicho kimelea na kulinda mfumo wa uongozi uliokwamisha
maendeleo ya haraka ya wananchi, jimboni Ilala na nchi nzima. Amesema mfumo huo
unakandamiza haki za wananchi na unachelewesha huduma za jamii zenye ufanisi
Hassanali ametaja baadhi ya maeneo ya
kushughulika nayo atakapokuwa mbunge kuwa ni ujenzi wa miundombinu ya barabara
jimboni, ukosefu wa ajira kwa vijana, mitaji ya biashara ndogo, elimu duni.
Amesema kuna mfumo wa ubaguzi
kwa wafanyabiashara akijitaja mwenyewe kuwa ingawa amezaliwa jimboni Ilala
anachukuliwa kama Mtanzania mwenye asili ya India.
Katika hafla ya uzinduzi wa
kampeni yake, pia walihudhuria viongozi wa dini, viongozi wa waendesha
bodaboda, machinga, soko la Karume.
Hassanali amekuwa mdhamini wa
Chadema kwa miaka 13 mfululizo na kugombea nafasi ya ubunge kwenye maeneo
matatu tofauti.
Habari hii
kwa hisani ya Mwanahali oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni