KWANI LOWASSA ANAKOSA GAN? SOMA HAPO KUJUA
Lowasa nimsamehe kwa
kosa gani?
Ngoja niwakumbusheni kidogo, Siku zile kashfa ya Richmond imezuka na
Lowasa amejiuzulu mimi binafsi mbali ya kuwa Rais wa MUCE nilikuwa Kamishna wa
TAHLISO.
Tulifanya kikao chetu Arusha na kuamua
kuandamana nchi Nzima ktk miji ya kivyuo yaani IRINGA, MOROGORO, MBEYA, DODOMA,
DAR, MOSHI, ARUSHA, NA MWANZA.
Mimi niliongoza maanda. ano ya Mbeya na Rais
wa Muhumbili wakati huo alikuja kuongoza ya Iringa. Katika maandamano yetu
tulidai mambo mawili,Mosi waliopiga
Richmond wapelekwe mahakamani, Pili tulitaka ikithibitika mali zao zitaifishwe
kufidia upotevu na kuboresha huduma za umeme.
Nakumbuka tulisikika sana ktk
medea na ilikuwa ni mara ya kwanza ktk nyakati zetu Wanazuoni kuandamana na
kutishia migomo kwa maslahi ya umma co matumbo yetu kama ilivo ada. Nini
kilitokea, Rais alikuja publicaly na kumsemea edo kuwa alikuwa kapata ajali ya
kisiasa na si mwizi,
Rais alienda kwa kampeni
Monduli uchaguzi wa 2010 akadai edo ni mtu safi mchapakazi, Kinana akiwa ktk
ziara zake akasema Lowasa safi Nyarando Mzigo, Walojiita makamanda wa kupinga
ufisadi ktk mradi wa Mwakyembe kama Lugola, Ole sendeka,Serukamba, nawengineo
wakageuka na kuwa kambi Lowasa ktk safari yake ya kutaka urais.
Upande wa pili serikali hiyohiyo nje ya Lowasa
ikaibariki mitambo ya Richmond ikawa Dowans na hatimaye Symbion iendelee
kutupigia kazi nchini, nakumbuka safari hii hata alokuwa kiongozi wangu Zito
alisema hapa hakuna shida itumike coz Ri hmond ni mchezo ulicgezwa na Ma ccm
ili kumalizana kisiasa wao kwa wao.
Hayo yakiendelea Kikwete akawapeleka Mahakamani mafisadi papa kama
Mramba, Yona na Mgonja. Wawili wamefungwa, Ivi kama mawaziri hawa wako jela kwa
ufisadi Lowasa anatafuta nn nje leo? Tena hata kesi tu hana?Najiuliza Lowasa
leo kahama chama na kwa hulka ya TANZANIA sote tunajua wezi, wachafu hata
majambazi hujibanza ccm ili wasishtakiwe au wahurumiwe maovu yao,
lakini Edo kawaambia tena na tena
Serikali safari hii akiwa nje ya ccm kuwa anayenituhumu kwa rushwa anipeleke
mahakamani wapi badala yake wanakuja na porojo kwa kumpatia nyaraka Mzee Slaa
akidai eti mkizitaka hizi mwende ikulu?
Yeye ikulu wamempa za nn badala
ya kupeleka mtuhumiwa mahakamani?Kwa mtu mwenye akili timamu zinazojitegemea
kama mimi nimekataa, Sitadanganywa kamwe, Lowasa kwa muktadha wa Richmond sio
fisadi kabisa, Anaedai namsafisha hajui, Wachafu ndo husafishwa,Kwa kuwa
naamini tuna haja ya kubadili mfumo wa utawala ili kubeba agenda zetu za
mabadiliko kama katiba ya wananchi, kwa kuwa edo kio gozi mzoefu anayependwa
ameamua kuwa upande wetu, basi atapewa kura c yangu tu bali na mamilioni ya
watazania.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni