MAANDAMANO "FEKI" YA CHADEMA YAMPONZA PAPARAZI WA GAZETI LA UHURU,ASHUSHIWA KIPIGO ,SOMA HAPO KUJUA
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la CCMChristopher Lissa akiwa na Kdai feki za Chadema alizokutwa nazo huku akiwa amechoka baada ya kudondoshewa kipigo |
MWANDISHI Christopher Lissa
wa Habari wa Gazeti linalotumika na Chama cha Mapinduzi CCM kueneza sera
za kipropaganda za chama hicho la UHURU ameambulia kipigo kutoka kwa watu wanaohisiwa ni wanachama
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.Anaandika
KAROLI VINSENT, endelea nayo.
Tukio hilo,limetokea leo kwenye Makao
Makuu ya Ofisi ya Chadema yaliyopo Kinondoni Jijini Dar es Salaam,pale ambapo
watu wanaojiita na kuitwa ni wanachama wa Chadema wakiwa zaidi 20 walipoandamana
mpaka kwenye ofisi hizo wakitaka kurudisha Kadi za Chadema kwa kile
wanachokisema kuwa-
Mgombewa wa
Urais wa Chadema ambaye anaungwa mkono na Vyama vinavyounda Ukawa,Edward
lowassa wakisema eti ni mdini kutokana na kauli alizozitoa kwenye kanisa moja
nchini.
Kauli hiyo
ni ile ya Lowassa alipowataka waumini wa
Kanisa la kulutheli wamuombee ili ashindi Urais mwaka huu ili Rais atoke upande
wa dhehebu hilo.
Kwa Mujibu wa Mtoa taarifa wetu aliyoko
ndani ya Chadema ameuambia Mtandao huu kuwa kilichomponza Paparazi huyo wa
Gazeti la CCM ni ukaidi wake kwa walinzi wachadema pamoja na kuwachukiza
wanachama wa chama hicho walioko ofisi hapo.
Amesema Mara vijana hao walipofika Ofisni hapo, walinzi wa Chadema waliwapokea kwa amani na kutaka kuwasikiriza nini kilicho wasibu. ambapo vijana hao wakasema wamekuja ofisini hapo
kurudisha kadi za Chama hicho ndipo walinzi hao wakawataka watoe kadi hizo,
Mara baada
ya kutoa kadi hizo za Chadema zikabainika ni Kadi feki kwa kuwa zinamakosa kibao ambayo yanamuondolea
mtu uachama,
Chanzo chetu hicho kikasema Makosa yaliyokuwepo
kwenye kadi hizo ni kukosa picha wala sahihi ya kiongozi yeyote wa
Chadema kwaanzi ngazi ya Kata huku zengine zikiwa ni zakutengeneza maana ni
feki.
Kuibuka kwa wananchama hao “Feki” kunakuwa
ni mwendelezo wa vijana wanakodiwa na
Mgombea moja Ubunge kupitia CCM ambaye anatokea Jimbo mojawapo Mkoani
Dar Es Salaam huku akidaiwa kushirikiana na Mtoto wa Kigogo mmoja kutoka ndani
ya CCM pamoja na Baadhi ya Wahariri wa magazeti
matatu ya kila siku,
Taarifa zinasema ya lengo ya maandamano hayo
ni kutaka kuwachanganya Watanzania katika kipindi hichi kigumu cha Kampeni ili
Chadema Kionekane kama kunamgogoro .
“Ujue
sikifichi CCM wamechanginikiwa sana kwahiyo wanatumia kila aina ya njia
kuhakikisha wanabaki madarakani,wamewatumia wakina Dk Slaa wameona mambo bado
magumu”
“Wametumia
sera ya Udini bado, wamekuja na sera ya Afya imewashinda maana mtu wanayemtuhumu
ni mgonjwa nafanya kazi kwa nguvu na sahivi yupo mikonani,yaani wanapagawa sana
jamani ila wananchi wapuuze ujinga huu”amesema kigogo mmoja wa Chadema
MKANDA MZIMA UTIZAME HUU HAPA
Katika hali ya kushangaza leo makao makuu ya chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA kimetokea kihoja cha karne baada ya watu wanaodhaniwa kuwa wanachama wa chama cha mapinduzi kufanya maandamano ambayo hayakufanikiwa na badala yake kusababisha mwandishi wa gazeti la UHURU kuingia matatani baada ya kuonekana kuambatana na vijana hao waliokuwa wanataka kuandamana kutokumtaka Edward lowasa.
Majira ya saa nne asubuhi vijana kadhaa ambao walikuwa wamevalia sare za chama cha CHADEMA na mabango kadhaa walionekana wakikatiza makao makuu ya chama hicho kwa mithili ya maandamano huku wakiwa wanachukuliwa picha na mwandishi wa gazeti la UHURU pamoja na mpiga picha wa Television ya STAR TV ambapo baada ya kufika makao makuu ya chama hicho walinzi pamoja na maafisa wa cham hicho walijipanga na kuwazunguka vijana hao ambao baadhi walikuwa na boda boda hali iliyowafanya vijana hao kutawanyika kwa kukimbia na kuvua t shirt za chama hicho ambazo walikuwa wamevalia juu ya nguo nyingine.
Baadhi ya kadi ambazo inadaiwa kukutwa nazo mwandhishi huyo |
Katika purukushani hizo waandishi waliokuwa wanawasindikiza waandamanaji hao akiwemo mwandishi wa gazeti la uhuru CHRISTOPHER LISSA pamoja na mpiga picha wa STAR TV waliwekwa chini ya ulinzi wa makamanda wa chama hicho kuwa kuhusishwa na kupanga tukio hilo ili wapate habari kuwa kuna maandamano lengo likiwa ni kukichafua chama hicho.
Mara baada ya kuwekwa chini ya ulinzi akiwemo mmoja kati ya vijana ambao alionekana kuchoka (TEJA) naye alikamatwa ambapo katika maelezo yake alikiri kupokea shilingi elfu kumi pamoja na T-SHIRT ya CHADEMA kutoka kwa vijana hao kwa lengo la kuambatana nao katika maandamano hayo ambayo hayakuwa halali.
Mwandishi wa gazeti la uhuru CHRISPHER LISSA wakati akitoa maelezo kwa maafisa wa chadema alisema kuwa yeye alipokea ujumbe mfupi wa maelezo kuwa kutakuwa na maandamano kuelekea CHADEMA kupinga alichofanyiwa DK SLAA ambapo kwa mujibu wa mwandishi huyo aliamua kufikisha ofisini na kupangiwa kazi hiyo ya kufanya coverage katika maandamano hayo ya leo.
Kwa mujibu wake anasema kuwa leo aliamua kufikia kinondoni kituo cha manyanya kutafuta hao waandamaji na ndipo alipokutana na wenzake wa STAR TV na kisha watu ambao walikuwa wamepanga kuandamana kwalifika wakiwa na gari na kushuka na kuanza kupeana T-SHIRT za CHADEMA huku wakiwa ni kama wageni wa eneo hilo wakiulizia makao makuu ya chama kwa watu wengine.
Anasema kuwa baada ya kugawiana nguo za chadema huku wakiwa hawasemi wao ni kina nani na wametumwa na nani walianza kusogea makao makuu ya chama hicho huku wakiimba na kushiria kuwa kua kitu wanakidai,ambapo ndipo maafisa wa chama waliamua kuwaweka kati na kufanikiwa kuzima tukio hilo.
Akizngumza na wanahabari afisa wa chama hicho BONIFACE JACOB amesema kuwa chama kilipata taarifa siku tatu nyuma kuwa kuna vikao vinakaa chini ya viongozi wawili wa CCM ambao amewataja kuwa ni PAUL MAKONDA ambaye ni mkuu wa wilaya ya kinondoni pamoja na mgombea ubunge wa jimbo la ubungo DIDAS MASABUR,vikao ambavyo vilifanyika kurasini na ndipo chama kilijipanga kwa tukio hilo la leo.
Kwa mujibu wa afisa huyo anasema kuwa mwandishi huyo wa UHURU anahisiwa kushiriki kupanga maandamano hayo kutokana na kukutwa na kadi zaidi ya 20 feki za chama hicho ambazo walijipanga kujifanya kama zimerudishwa na wanachama hao kadi ambazo mwandishi huyo amekana kuhusika nazo.
JOHN MNYIKA AKIZUNGUMZIA KIHOJA HICHO
Akizungumzia kihoja hicho leo Naibu katibu mkuu wa CHADEMA ndugu JOHN MNYIKA amesema kuwa wanahabari huu ni muda wa kuwa makini sana na kukwepa kutumika na wanasiasa kwa maslahi yao binafsi kwani inaweza kuwagharimu hata maisha na baadae wanasiasa wanakuwa wametimiza lengo lao.
Mnyika anasema kuwa zipo mbinu chafu ambazo zinachezwa na wasiasa hasa wa chama cha mapinduzi kuwapanga vijana na kuwataka waandamane kwa malipo na kujifanya wao ni wanachadema jambo ambalo amesema kuwa ni kuwaumiza vijana hao kwani wamekuwa wakiishia kupata vipigo kutoka kwa wananchi ambao wanachukizwa na vitendo hivyo.
CHINI MWANDISHI WA UHURU AKIFAFANUA
CHINI MWANDISHI WA UHURU AKIFAFANUA
HABARII NA EXAUDI MTEI
Hakuna maoni
Chapisha Maoni