SHERIA YA MITANDAONI KUFUTWA,WANAHARAKI WAKIMBILIA MAHAKAMANI,SOMA HAPO KUJUA
Mkurugenzi wa THRDC, Onesmo Olengurumwa |
MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) kwa kushirikiana
na mashirika mengine ya kutetea haki za binadamu leo wamefungua kesi ya
Kikatiba kupinga baadhi ya vipengele katika Sheria ya Makosa ya Mitandao. Anaandika Sarafina Lidwino …
(endelea).
Vipengele vinavyopigwa ni kifungu cha 4,
5 na 45 (4) cha Sheria ya Makosa ya Mitandaoni ambacho kinazuia haki ya kupata
na kutoa taarifa ambacho kinakinzana na Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamuhuri ya
Muungano Tanzania.
Vipengele vingine ni Kifungu cha 6, 7, 8,
10, 11, 14, 19, 21 na 22 ambavyo vina maneno yasiyo na tafsiri na kuweza
kusababisha tafsiri mbaya kwa watekeleza sheria na hivyo kupelekea uvunjifu wa
haki za binadamu ambavyo vinakiuka Ibara ya 17 ya Katiba.
Vifungu vya 31,33,34,35 na 37 vya sheria
hiyo vinatoa mamlaka kwa Polisi kufanya upekuzi bila idhini ya Mahakama
hivyo ni uvunjufu wa haki za binadamu na inakinzana na Ibara ya 16 ya Katiba.
Vipengele vingine, Kifungu cha 38 cha
sheria hiyo kinanyima haki ya mtu kusikilizwa na Mahakama huvyo inakinzana na
Ibara ya 13 (6) ya Katiba pamoja na kifungu cha 47 (1) cha sheria hiyo
kinanyima Polisi kufanya kazi zao kama ilivyo katika Sheria hii.
Hatua hiyo ya kufungua kesi imekuja
baada ya Aprili mwaka huu Bunge kupitisha sheria ya makosa ya mitandaoni
(Cybercrime Act 2015) ambapo watetezi wa haki za binadamu hapa nchini kwa
kushirikiana na mashirika ya Kimataifa yalifanya uchambuzi na kubaini kuwa
baadhi ya vipengele katika sheria hiyo vilikuwa na mapungufu makubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari
Jijini Dar es Salaam nje ya Mahakama Kuu, Mkurugenzi wa THRDC, Onesmo
Olengurumwa amesema uchumbuzi uliofanyika ulibaini kuwa sheria iliyopitishwa ni
mwiba kwa uhuru wa vyombo vya habari, haki ya falagha na haki ya watu kupata
taarifa na kutoa maoni.
Olengurumwa amedai, baada ya wadau hao
kuyagundua makosa hayo ambayo yalikuwa yanafinya haki za binadamu waliamua
kutoa maoni ambayo serikali iliahidi kuyafanyia marekebisho. Lakini licha
ya sheria hizo kufanyiwa marekebisho bado kunavipengele ambavyo vinamakosa.
Ndani ya sheria hizo waligundua kuwa
endapo sheria hiyo itaendelea kutumika itakuwa imekiuka haki za binadamu kama,
Uhuru wa habari, uhuru wa maoni, uhuru wa kutafuta habari, Haki ya faragha,
Haki ya kuifikia Mahakama na Haki ya kusikilizwa.
Anasema Mei 22 mwaka huu Serikali
ilitangaza kutumika sheria ya makosa mitandaoni pasipo kufanyiwa marekebisho
ambayo yalipendekezwa na wadau wa haki za binadamu.
“Ikumbukwe kuwa kabla ya sheria hiyo
kupitishwa Mashirika yasiyopungua 55 mwaka huu chini ya uratibu wa THRDC
yalimwandikia barua Rais Kikwete ya kumsihi asitie saini kabla ya sheria hiyo
kufanyiwa marekebisho lakini pia ilipuuzwa”. anasema Olengurumwa.
Aidha amesema, kutokana kwamba
sheria hiyo imeanza kutumika THRDC pamoja na mashirika mbalimbali ya Haki za
Binadamu wakiungana na jopo la wanasheria saba tumeamua kumuunga mkono na
kufungua kesi kupitia wakili wa kujitegemea Jebra Kambole ambaye ndiye
mlalamikaji katika kesi hiyo katika kuhakikisha kuwa baadhi ya vipengele katika
sheria hiyo vinapigwa.
“Ikumbukwe kuwa taratibu za
kisheria zinapendelea zaidi kesi kama hizi zifungukuwe na mtu binafsi na
si shirika hivyo tunamuunga mkono hadi mwisho. Na endapo Mahakama
itashidwa kutenda haki katika kesi hii basi tutaipeleka mbele zaidi katika Mahakama
ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kupata utatuzi,” anasema Kambole.
Jopo la Mawakili hao saba ni, John
Seka, Massawe Fulgence, Harold Sungusia, Benedict Ishabakakaki, Jebra Kambole
(wakili wa kujitegemea), Boka Iyamuya, Neema Ndemno na Geremia Mtobesia ambapo
kesi imepewa jarada la Miscellaneous Civil Case namba 32 ya mwaka 2015.
Habari hii Kwahisania ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni