BABU DUNI AWATAKA WATANZANIA KUIPOTEZEA CCM NA KUCHAGUA UKAWA,SOMA HAPO KUJUA
Mgombea Mwenza wa Chadema kupitia UKAWA, JJuma Haji Duni akihutubia wananchi wa Segerea\
MGOMBEA Mwenza wa urais
kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema) Juma Duni Haji, amesema iwapo wananchi watamchagua
Edward Lowassa watajipa uhakika wa kuondokana na tatizo sugu la maji. Anaandika Pendo Omary … (endelea).
Duni ametoa ahadi hiyo leo wakati wa
ziara ya kampeni jimboni Segerea jijini Dar es Salaam alikohutubia na kuondoka
kwenda Zanzibar kuungana na mgombea urais wa Zanzibar kupitia CUF, Maalim Seif
Shariff Hamad aliyezindua kampeni leo.
Duni alitakiwa kufanya ziara katika majimbo
mengine ya Temeke na kigamboni lakini akashidwa kutokana na kuhitajika katika
mkutano wa kufungua kampeni za Serif visiwani Zanzibar.
Hivyo mikutano hiyo kuendeshwa na
viongozi na makada wa vyama vya Ukawa wakiwemo Makamo Mwenyekiti (Chadema)
Zanzibar, Said Issa Mohammed, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CUF Wilaya
ya Kinondoni, Blandina Masabwite, aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mkanyageni,
Pemba, Mohamed Mnyaa na Suzan Lyimo wa Chadema.
Amesema “Leo jua kali watu wanaugua
kipindupindu jijini Dar es Salaam. Ni kwa sababu wanakunywa mavi (maji
yaliyochanganyika na kinyesi). Tutahakikisha jijini la Dar es Salaam watu
hawanywi mavi. Tatizo la maji litakwisha. Tutashirikiana na halmashauri,”
amesema Duni.
Ameahidi kuwa serikali itakayotokana
na Ukawa itasimamia huduma za afya na elimu kutolewa kwa ufanisi, pamoja na
kupunguza kodi kwa lengo la kuvutia ulipaji wa hiyari na kuhakikisha jiji
linaondokana na uchafu.
“Tukiingia madarakani matibabu ya
mama na mtoto yatakuwa chini ya gharama za serikali, kupitia mpango wa bima,”
amesema Duni.
Aidha, amesema “watoto wa masikini
watasoma bila Malipo kuanzia darasa la kwanza mpaka watakaposhidwa wenyewe,”
amesema Duni.
Mgombea ubunge jimbo la
Segerea anayewakilisha Ukawa, Julius Mtatiro (CUF) amesema akichaguliwa kuwa
mbunge atashirikiana na wananchi kuimarisha miundombinu ya barabara na
kusimamia huduma bora za afya, maji na kuanzisha mifuko ya kuweka na kukopa
ngazi ya Kata.
“Baada ya taarehe 25 Oktoba nitahakikisha
mbunge wenu anakuwa na ofisi hapahapa Segerea. Nitaanzisha mifuko ya kata ya
kuweka na kukopa ya vijana na akinamama,” amesema Mtatiro. Jimbo hilo halina
ofisi ya mbunge.
Blandina amesema wanawake na watoto
watafurahi kupata serikali inayowaangalia kwa kuwa hali zao ziko hoi. “Tunataka
serikali itakayolinda maslahi yetu mama na watoto…. itakayoleta ajira kwa
vijana.”
Habari hii kwa hisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni