ASKOFU KILAINI AIBUKA NA KUMBAMIZA DK SLAA,BOFYA HAPO KUJUA
PICHANI NI ASKOFU KILAINI PICHA NA MAKTABA |
NA KAROLI
VINSENT
KILE kinachoonekana
ni kama wanasiasa na viongozi wa dini wamechoka na upotoshaji uliotolewa na
aliyewai pata kuwa Katibu mkuu wa
Chadema,Dokta Wilbroad Slaa juu ya madai
aliyosema maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini wamehongwa,
Hayo yamethibitishwa na Askofu
Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini kuibuka na kumshabulia Dokta
Slaa na kusema anapotosha umma na akawataka watanzania kumpuuza.
Akizungumza Mkoani hapa, Askofu
Kilaini amesema Kauli aliyoitoa Dokta Slaa kuwa Maaskofu 30 wa kanisa katoliki wamenunuliwa ni
kauli ambayo imemsikitisha akidai kuwa maaskofu wa kanisa katoliki hawanunuliki.
“Kwa kweli kauli hii imesikisikitisha
nisingetegemea Dokta Slaa kutoa kauli hiyo huku akizingatia yeye aliwai kuwa Katibu
mkuu Baraza la Maaskofu nchini,anajua jinsi kanisa linavyofanya kazi ,kwani
maaskofu wa kanisa katoliki hawanunuliki hata kidogo”amesema Kilaini.
Amesema Matamko
anayotoa Dokta Slaa ni mabaya sana katika jamii kwani yanaweza kuliingiza taifa
kwenye matatizo huku akitolea mfano uchaguzi wa mwaka 2000 ,akisema katika
kuepuka machafuko huku Zanzibar kwa
kusema viongozi wa dini walifanya jambo jema katika kutuliza machafuko hayo
kwakuungana dini zate ikiwemo hata za kiislam na kusaidi kutuliza fujo.
Askofu Kilaini ambaye aliwai kuwa
Katibu mkuu wa baraza la Masskofu nchini TEC amebainisha kuwa kama kanisa lizima lishikilie
maadili na kuombea amani Taifa huku akiimtadhalisha Dokta Slaa kuwa makini na
kauli zake kwani zinaweza kuchochoa vurugu nchini.
Vilevile Askofu huyo akawataka
wanasiasa kuepuka kutumia dini kama nyenzo ya kukubalika kwa jamii na
kuwasisitiza kutumia hoja katika kuwashawishi watanzania.
Kuibuka huko kwa Askofu Kilaini kuna
kuja siku moja kupita baada Bilionea maarufu Afrika Rostam Azizi kumvaa Dokta
Slaa kwa kusema ni mpotoshaji na muungo baada kutuhumiwa kuwa anaifadhili
Chadema.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni