TGNP YAWAPIGA MSASA WANAWAKE NCHINI,YATOA DARASA TOSHA SOMA HAPO KUJUA
ISHWA JUU YA SHERIA NA MAKOSA YA MITANDAO
Afisa Sheria wa Wizara ya Mawasiliano, Eunice Masigati akizunzungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na sheria za makosa ya mitandao, ambapo sheria hii itatumia Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar wakati wa Tamasha la mtandao wa wanawake na katiba na uchumi linaloendela TGNP jijini Dar es Salaam.
Afisa Mawasiliano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Melkizdeck Karol akiwaelimisha waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya usalama wa sheria za mitandao wakati wa Tamasha la mtandao wa wanawake na katiba na uchumi linaloendela TGNP jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Afisa Sheria wa Wizara ya Mawasiliano, Eunice Masigati.
Afisa Sheria wa Wizara ya Mawasiliano, Eunice Masigati akimsikiliza waandishi wa habari wakichangia mada kuhusiana na sheria za makosa ya mitandao wakati wa Tamasha la mtandao wa wanawake na katiba na uchumi linaloendela TGNP jijini Dar es Salaam.
Wanahabari wakimsilikiza kwa makini Afisa Sheria wa Wizara ya Mawasiliano, Eunice Masigatiwakati wa Tamasha la mtandao wa wanawake na katiba na uchumi linaloendelea TGNP jijini Dar es Salaam.
Wanawake
kote nchini wametakiwa kutosubiri kuwezeshwa bali wajiwezeshe wewenywe ili
waweze kujikomboa kiuchumi na kuwa na maendeleo yatakayo wawezesha kujikwamua
kiuchumi.
Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam
na Mbunge mstaafu wa viti maalumu wa mkoani Songea Devotha Likokola katika
tamasha la wanawake linalo endelea katika ofisi za TGNP mtandao Mabibo, ambapo
amesema wakati uliopo sasa si wanawake kusubiri kuletewa mabadiliko bali
wanatakiwa kujishungulisha kwa kujiunga na vikundi mbalimbali ili waweze
kujikomboa kiuchumi.
Ameongeza kuwa wanawake wanatakiwa
kuungana kwa pamoja ili kuweza kuwezeshwa kiuchumi na serikali, kwani nguvu ya
mtu mmoja haiwezi kuleta maendeleo kwa wanawake wote bali ni kwa kuunda vikundi
na kuwa kitu kimoja ili kuweza kujikomboa kiuchumi.
Likokola ameongeza kuwa wanawake
wanatakiwa kutokuwa waoga kujaribu kujishugulisha katika shuguli mbalimbali kwa
kudhani kwamba hawawezi kufanya shughuli hizo na kujenga dhana kuwa wanaume
pekee ndio wanaoweza kufanya shughuli za kimaendeleo katika jamii na kuleta
maendeleo kwani hata wanawake nao wanaweza kwa juhudi za kujishugulisha kwa
bidii.
Kwa upande wake Neema Masanja alisema
kuwa yeye kama mwanamke hana dhana ya kusubiri kuwezeshwa kwani ameisha
jiwezesha mwenywe kwa kujiunga na vikundi vya Vikoba ambavyo vime muwezesha
kuendesha shughuli zake za maendeleo bila kutegemea kuwezeshwa.
Aidha ametoa wito kwa wanawake wenzake
kutokuwa na dhana ya kusubiri kuwezeshwa kwani Dunia ya sasa ni ya tofauti sana
na wanawake wanatakiwa kutojimbweteka kusubiri kuletewa nyumbani na wanaume wao
bali wanaweza kujiunga na vikundi mbalimbali vya Vikoba ili kuweza kupata
mikopo ya kuweza kufanya biashara zao bila kuwa tegemezi.
Habari hii imeandikwa na Moshi Shabani Mallema, DAR ES SALAAM
Hakuna maoni
Chapisha Maoni