HABARI ILIYOTIKISA JIJI- NI LOWASSA NI LOWASSA,ALITEKA JIJI SAA TANO,OFISI ZA UMMA ZASIMAA KUPISHA GHARIKA YA LOWASSA,TIZAMA HAPO KUJUA
EDWARD Lowassa tayari amechukua fomu za Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) za kugombea urais katika kura itakayopigwa Oktoba 25 mwaka huu,
siku ya uchaguzi mkuu nchini. Anaandika
Jabir Idrissa …
(endelea).
Lowassa
ambaye ni waziri mkuu aliyejiuzulu Februari 2008, kuihifadhi Serikali ya CCM
iliyokumbwa na kashfa ya mkataba wa Richmond, amechukua fomu hizo mchana leo
akifuatana na viongozi wote wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Fomu hizo amezichukua kwa tiketi ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CAHDEMA) ambacho kimepewa dhamana na UKAWA
kuwakilisha umoja huo katika kampeni ya kukiondoa madarakani Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Katika uchukuaji wa fomu, Lowassa
alikuwa na mgombea wake mwenza, Juma Duni Haji, mwanasiasa gwiji aliyehamia
Chadema akitoka Chama cha Wananchi (CUF) kwa lengo la kutimiza masharti ya
UKAWA katika kusimamisha mgombea mmoja.
Duni alikuwa makamu mwenyekiti wa
CUF, waziri wa Mawasiliano na Miundombinu na alishateuliwa kugombea kiti cha
uwakilishi, jimbo la Bububu, mjini Zanzibar.
Viongozi waliofuatana na msafara wa
Lowassa na Duni, ni wenyeviti wa vyama hivyo vinavyoshirikiana akiwemo Dk.
Emmanuel Makaidi wa Chama cha National League for Democracy (NLD) na Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe.
Kiongozi mwingine ni James Mbatia,
ambaye ni mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi. Wenyeviti wote hao ni wanatambuliwa kama
wenyeviti wenza wa UKAWA.
Viongozi wengine ni makatibu
wakuu wa vyama hivyo wakiongozwa na Maalim Seif Shariff Hamad wa CUF ambaye pia
ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Pia alikuwepo Twaha Taslima,
aliyeteuliwa jana na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF kuongoza Kamati ya
Muda ya uongozi itakayodumu kwa miezi sita ikifanya kazi za mwenyekiti na
makamu ambao wote wamejiuzulu.
Mwenyekiti alikuwa Profesa
Ibrahim Lipumba aliyejiuzulu Agosti 5 kwa kudai hawezi kuendelea kushika
wadhifa huo kutokana na tofauti na wenzake. Duni alijiuzulu ili kuwezesha
kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Lowassa.
Msafara wa Lowassa na Duni ukisindikizwa
na viongozi wote hao ulianzia Ofisi Kuu za CUF Buguruni, jijini Dar es Salaam
ambako tangu alfajiri leo wanachama walikusanyika kusubiri kushuhudia.
Eneo hilo lilikuwa kivutio kwa
muda wote mpaka ilipofika saa 5.20 msafara ulipoanza safari ya kwenda Tume ya
Taifa ya Uchaguzi makao makuu, jengo lililokuwa maskani ya Tume ya Mabadiliko
ya Katiba, mtaa wa Ohio.
Mkusanyiko mkubwa wa watu
Buguruni ulikuwa kama marudio ya jana siku ambayo Lowassa alifika ofisi hizo na
kuhutubia Baraza Kuu la Uongozi la CUF lililokuwa na kikao cha dharura. Lowassa
pia alihutubia kwa muda mfupi wananchi waliokuwepo.
UKAWA umeimarika kwa kuingia
Lowassa ambaye amefuatwa na makada kadhaa wa CCM wakiwemo waliokuwa wabunge,
James Lembeli (Kahama), Dk. Makongoro Mahanga (Segerea), Ester Bulaya (Viti
Maalum) na Goodluck ole Medeye (Arumeru Magharibi) ambaye pia alikuwa Naibu
Waziri wa Ardhi.
Wakati watu walijazana Buguruni huku
kukiwa na utitiri wa walinzi wa vyama vyote hivyo, shamrashamra zilizidi
walipochomoza polisi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala akiwa na
askari wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU).
Msafara wao uliingia ndani ya
uwanja wa ofisi kuu za CUF na kamanda kushuka na kupanda walikokuwa viongozi
wakuu ambao walikuwa wakimsubiri Lowassa kuwasili.
Kuliibuka hofu ya namna Fulani,
hasa kwa kuwa kabla ya hapo kulishasikika tamko la Kamishna Suleiman Kova wa
Kanda Maalum Dar es Salaam, kwamba hawakuruhusu maandamano katika tukio hilo la
mgombea wa Chadema kuchukua fomu NEC.
Hata hivyo, baada ya majadiliano
marefu, Kamanda wa Ilala aliridhia kuongoza msafara wa viongozi wakuu wa UKAWA
kuondoka kwenda makao makuu ya NEC.
Msafara huo ulilazimika kwenda mwendo
wa pole kutokana na watu wengi kujitokeza barabarani kila ulipopita ukitumia
barabara ya Uhuru kupitia Kariakoo.
FAHIDI PICHA ZOTE HAPO TUKOA ZIMA HILO HAPO
Hali ilivyokuwa katika barabara ya Bibi Titi na Morogoro.
Wafuasi wa vyama vinavyounda Ukawa wakiwa kwenye gari kuelekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa ajili ya kumsindikiza Mgombea Urais kupitia Ukawa, Edward Lowassa.
…umati uliofurika.
Wafuasi wa vyama vyote wakiwa juu ya gari lao kuelekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumsindikiza Lowassa.
Gari la Mhe. Lowassa likisindikizwa kuelekea Makao makuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kinondoni mara baada ya kuchukua fomu.
Wananchi barabarani wakimlaki Lowassa kwa kuonesha ishara ya Chadema.
Ulinzi ulivyoimarishwa.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrosia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe alipowasili katika ofisi za Chama Cha wananchi (CUF) asubuhi ya leo kabla ya msafara kuanza.
James Lembeli akisalimiana na mmoja wa viongozi wanaounda Ukawa.
Kamanda mkuu wa kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) Ukonga akibadilisha neno na askari mwenzake kama inavyoonekana pichani.
Ester Bulaya (aliyeko juu ya gari kulia akiwa kwenye msafara huo.
Taswira ya msafara wa Lowasa.
Maelfu ya wananchi wa jiji la Dar kumsindikiza kuchukua fomu mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa kwenda NEC kuanzia ofisi za CUF.
Hatimaye mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Waziri Mkuu mstaafu Edward Ngoyai Lowassa leo amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Awali, mgombea huyo alianzia Makao Makuu ya Chama cha Wananchi (CUF), Buguruni, Dar es Salaam kisha kuelekea Tume yaTaifa ya Uchaguzi kwa kupitia barabara ya Uhuru, Bibibti Mohamed hadi Makao Makuu ya Tume hiyo.
Baada ya hapo, msafara wake ulipititia Barabara ya Ocean Road kisha Umoja wa Mataifa, Ally Hassan Mwinyi hadi Makao Makuu ya CHADEMA yaliyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Katika msafara huo, umati mkubwa wa wapenzi na wakereketwa wa mgombea huyo walijitokeza kumsindikiza .
Wananchi wamejitokeza kwa wingi leo kumsindikiza Edward Lowasa kwenda kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA).
Msafara ulianza rasmi kutoka katika ofisi za chama hicho kupitia ofisi za CUF na kuhitimisha katika ofisi za NEC Taifa.
Wananchi wakimsindikiza Waziri mkuu msaafu Edwald Lowassa (CHADEMA) wakati akielekea kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Demokrasioa na Maendeleo (CHADEMA) wakitokea ofisi za chama hicho kupitia ofisi za CUF na kuhitimisha katika ofisi za NEC jijini Dar es Salaam leo.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Maoni 1
Nmeipenda hii...Nawaomba wote walojitokeza kutunza shahada zao
Chapisha Maoni