Zinazobamba

HABARI ILIYOTIKISA JIJI- NI LOWASSA NI LOWASSA,ALITEKA JIJI SAA TANO,OFISI ZA UMMA ZASIMAA KUPISHA GHARIKA YA LOWASSA,TIZAMA HAPO KUJUA


EDWARD Lowassa tayari amechukua fomu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) za kugombea urais katika kura itakayopigwa Oktoba 25 mwaka huu, siku ya uchaguzi mkuu nchini. Anaandika Jabir Idrissa … (endelea).
Lowassa ambaye ni waziri mkuu aliyejiuzulu Februari 2008, kuihifadhi Serikali ya CCM iliyokumbwa na kashfa ya mkataba wa Richmond, amechukua fomu hizo mchana leo akifuatana na viongozi wote wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
         Fomu hizo amezichukua kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CAHDEMA) ambacho kimepewa dhamana na UKAWA kuwakilisha umoja huo katika kampeni ya kukiondoa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM).
          Katika uchukuaji wa fomu, Lowassa alikuwa na mgombea wake mwenza, Juma Duni Haji, mwanasiasa gwiji aliyehamia Chadema akitoka Chama cha Wananchi (CUF) kwa lengo la kutimiza masharti ya UKAWA katika kusimamisha mgombea mmoja.
            Duni alikuwa makamu mwenyekiti wa CUF, waziri wa Mawasiliano na Miundombinu na alishateuliwa kugombea kiti cha uwakilishi, jimbo la Bububu, mjini Zanzibar.
          Viongozi waliofuatana na msafara wa Lowassa na Duni, ni wenyeviti wa vyama hivyo vinavyoshirikiana akiwemo Dk. Emmanuel Makaidi wa Chama cha National League for Democracy (NLD) na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
             Kiongozi mwingine ni James Mbatia, ambaye ni mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi. Wenyeviti wote hao ni wanatambuliwa kama wenyeviti wenza wa UKAWA.
Viongozi wengine ni makatibu wakuu wa vyama hivyo wakiongozwa na Maalim Seif Shariff Hamad wa CUF ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
       Pia alikuwepo Twaha Taslima, aliyeteuliwa jana na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF kuongoza Kamati ya Muda ya uongozi itakayodumu kwa miezi sita ikifanya kazi za mwenyekiti na makamu ambao wote wamejiuzulu.
Mwenyekiti alikuwa Profesa Ibrahim Lipumba aliyejiuzulu Agosti 5 kwa kudai hawezi kuendelea kushika wadhifa huo kutokana na tofauti na wenzake. Duni alijiuzulu ili kuwezesha kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Lowassa.
          Msafara wa Lowassa na Duni ukisindikizwa na viongozi wote hao ulianzia Ofisi Kuu za CUF Buguruni, jijini Dar es Salaam ambako tangu alfajiri leo wanachama walikusanyika kusubiri kushuhudia.
             Eneo hilo lilikuwa kivutio kwa muda wote mpaka ilipofika saa 5.20 msafara ulipoanza safari ya kwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi makao makuu, jengo lililokuwa maskani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, mtaa wa Ohio.
Mkusanyiko mkubwa wa watu Buguruni ulikuwa kama marudio ya jana siku ambayo Lowassa alifika ofisi hizo na kuhutubia Baraza Kuu la Uongozi la CUF lililokuwa na kikao cha dharura. Lowassa pia alihutubia kwa muda mfupi wananchi waliokuwepo.
                UKAWA umeimarika kwa kuingia Lowassa ambaye amefuatwa na makada kadhaa wa CCM wakiwemo waliokuwa wabunge, James Lembeli (Kahama), Dk. Makongoro Mahanga (Segerea), Ester Bulaya (Viti Maalum) na Goodluck ole Medeye (Arumeru Magharibi) ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Ardhi.
          Wakati watu walijazana Buguruni huku kukiwa na utitiri wa walinzi wa vyama vyote hivyo, shamrashamra zilizidi walipochomoza polisi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala akiwa na askari wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU).
              Msafara wao uliingia ndani ya uwanja wa ofisi kuu za CUF na kamanda kushuka na kupanda walikokuwa viongozi wakuu ambao walikuwa wakimsubiri Lowassa kuwasili.
              Kuliibuka hofu ya namna Fulani, hasa kwa kuwa kabla ya hapo kulishasikika tamko la Kamishna Suleiman Kova wa Kanda Maalum Dar es Salaam, kwamba hawakuruhusu maandamano katika tukio hilo la mgombea wa Chadema kuchukua fomu NEC.
               Hata hivyo, baada ya majadiliano marefu, Kamanda wa Ilala aliridhia kuongoza msafara wa viongozi wakuu wa UKAWA kuondoka kwenda makao makuu ya NEC.
          Msafara huo ulilazimika kwenda mwendo wa pole kutokana na watu wengi kujitokeza barabarani kila ulipopita ukitumia barabara ya Uhuru kupitia Kariakoo.

   
FAHIDI PICHA ZOTE HAPO TUKOA ZIMA HILO HAPO 


Hali ilivyokuwa katika barabara ya Bibi Titi na Morogoro.
3.Wafuasi wa vyama vinavyounda ukawa wakiwa kwenye gari kuelekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kwa ajili ya kumsindikiza Mgombea Urais kupitia Ukawa,Edward Lowassa.
Wafuasi wa vyama vinavyounda Ukawa wakiwa kwenye gari kuelekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa ajili ya kumsindikiza Mgombea Urais kupitia Ukawa, Edward Lowassa.
4...umati uliofurika .
…umati uliofurika.
5.Harakati za kuelekea kusindikiza mgombea Urais zikiendelea barabra ya Bibi Titi.
Harakati za kuelekea kusindikiza mgombea Urais zikiendelea barabara ya Bibi Titi.
6.Wafuasi wa vyama vyote wakiwa juu ya gari lao kuelekea tume ya Taida ya Uchaguzu NEC kumsindikiza Lowassa.
Wafuasi wa vyama vyote wakiwa juu ya gari lao kuelekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumsindikiza Lowassa.
7.Gari la Mhe.Lowassa likisindikizwa kuelekea Makao makuu ya Chama Cha Demokrosia na Maendeleo (CHADEMA) Kinondoni mara baada ya kuchukua fomu.
Gari la Mhe. Lowassa likisindikizwa kuelekea Makao makuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kinondoni mara baada ya kuchukua fomu.
8.Wananchi barabarani hali ilivyokuwa wakimlaki Lowasa kwa kuonesha ishara ya Chadema.
Wananchi barabarani wakimlaki Lowassa kwa kuonesha ishara ya Chadema.
9.Ulizi yluviimalika.
Ulinzi ulivyoimarishwa.
10Mnyekiti wa Chama cha Demokrosia na Maendeleo,Freeman Mbowe alipowasili katika ofisi za Chama Cha wananchi CUF asubuhi msafara ulipoanzia.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrosia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe alipowasili katika ofisi za Chama Cha wananchi (CUF) asubuhi ya leo kabla ya msafara kuanza.
11.James Lembeli akisalimiana na mmoja wa viongozu wanaounda Ukawa.
James Lembeli akisalimiana na mmoja wa viongozi wanaounda Ukawa.
12.kamanda  mkuu  wa  kikosi cha kutuliza Ghasia FFU Ukonga akibadilisha jambo  na  mlinzi wake  wa  karibu kama inavyoonekana pichani
Kamanda mkuu wa kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) Ukonga akibadilisha neno na askari mwenzake kama inavyoonekana pichani.
13.Ester Bulaya(aliyeko juu ya garu kulia akiwa kwenye msafara huo.
Ester Bulaya (aliyeko juu ya gari kulia akiwa kwenye msafara huo.
14.Taswila ya msafara wa Lowasa.
Taswira ya msafara wa Lowasa.
11856528_766736266770683_4263750936932267814_o Maelfu ya wananchi wa jiji la Dar kumsindikiza kuchukua fomu mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa kwenda NEC kuanzia ofisi za CUF.

Hatimaye mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Waziri Mkuu mstaafu Edward Ngoyai Lowassa leo amechukua fomu ya kugombea  nafasi hiyo katika Makao Makuu  ya Tume  ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Awali, mgombea huyo alianzia Makao Makuu ya Chama cha Wananchi (CUF), Buguruni, Dar es Salaam  kisha kuelekea Tume yaTaifa ya Uchaguzi kwa kupitia barabara ya Uhuru, Bibibti Mohamed  hadi Makao Makuu  ya Tume hiyo.
Baada ya hapo, msafara wake ulipititia Barabara ya Ocean Road  kisha Umoja  wa  Mataifa, Ally Hassan Mwinyi hadi   Makao Makuu ya CHADEMA yaliyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Katika msafara huo,  umati  mkubwa  wa  wapenzi  na wakereketwa  wa mgombea huyo walijitokeza  kumsindikiza .


Wananchi wamejitokeza kwa wingi leo kumsindikiza Edward Lowasa kwenda kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA).


Msafara ulianza rasmi kutoka katika ofisi za chama hicho kupitia ofisi za CUF na kuhitimisha katika ofisi za NEC Taifa.
























Wananchi wakimsindikiza Waziri mkuu msaafu Edwald Lowassa (CHADEMA) wakati akielekea kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Demokrasioa na Maendeleo (CHADEMA) wakitokea ofisi za chama hicho kupitia ofisi za CUF na kuhitimisha katika ofisi za NEC jijini Dar es Salaam leo.

Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline

Maoni 1

TWIGA SEC SCHOOL alisema ...

Nmeipenda hii...Nawaomba wote walojitokeza kutunza shahada zao