Zinazobamba

BREAKING NEWS,KUJIUZULU KWA LIPUMBA,CUF WAFIKIA MAAMUZI HAYA KWENYE NAFASI HIYO,SOMA HAPO KUJUA

????????????????????????????????????
pichani ni aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha CUF Profesa ibrahimu Lipumba picha na Maktaba

SIKU Chache kupita baada ya Profesa Ibrahimu Lipumba kutangaza kujiuzulu nafasi ya uwenyekiti ndani ya  Chama cha wananchi CUF, Hatimaye Chama hicho kimeunda kamati ya mda itakayodumu kwa miezi sita ili kusimamia  nafasi za uongozi .Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
               Hatua hiyo imetangazwa mda huu  Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa mkutano na waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika Kikao cha Dharula cha Baaraza la kuu la uongozi wa chama hicho kilichoitishwa kujadili hatua hiyo ya kujiuzulu Profesa Lipumba /.

           Ambapo Seif amesema katokana na Kanuni za CUF wamefikia kwa pamoja kuunda kamati maalum itakayosimamia chama kwa kipindi cha Miezi sita na baadae kufanya uchaguzi wa nafasi hiyo ya uenyekiti.
             Amesema Kamati hiyo itakuwa chini ya Katibu wa CUF ambaye ni yeye Maalim Seif na mwenyekiti wake atakuwa Mbunge wa Afrika Mashariki   Twaha Taslima na Kamati hiyo itakuwa na kazi ya kukijenga chama hicho,pamoja na kushirikiana na Vyama vyengine vinavyounda UKAWA  ambapo anadai itakuwa na jukumu lengine la  kuhakikisha wanaitoa CCM madarakani.

            Endelea kafutaitilia  FULLHABARI.BLOGS utapata taarifa kamili

Hakuna maoni