CCM YAZIDI KUFA,MADIWANI WAZIDI KUKIMBIA,WAPO NA MAMIA YA WANACHAMA,SOMA HAPO KUJUA
Mwenyekiti wa sasa wa CCM Mkoa wa Mwanza, Dk. Anthony Diallo |
HALI ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza si shwali baada
ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Charles Lugo (Fashion), na wanachama
zaidi ya 100 kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF). Anaandik Moses Mseti, Mwanza … (endelea).
Tukio hilo linakuja ikiwa ni
mwendelezo wa wimbi la wanachama wa CCM kuhamia upinzani hususani Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA.
Diwani na wanachama hao kutoka matawi
mbalimbali ya CCM, walieleza chanzo na sababu za kutimkia CUF, kuwa chama hicho
kimetawaliwa na vitendo vya rushwa, chuki na undugu kitendo kinachosababisha
kukosekana kwa demokrasia ya kweli.
Wamesema viongozi wa CCM kuanzia ngazi
ya chini hadi Taifa, wamekuwa wakitumia rushwa kushika madaraka na kusababisha
watu ambao ni wazalendo wenye nia dhabiti ya kuwatumikia wananchi kukosa haki
hiyo.
Wanachama hao wakiongozwa na diwani
huyo, walipokelewa leo na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CUF, Karume Jeremiah,
wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Chakechake, Nyamagana.
Akizungumzia tamko la wao kujiengua
CCM na kujiunga CUF, Fashion amesema wamefikia hatua hiyo kutokana na kuchoshwa
na vitendo alivyodai vya rushwa kwenye uchaguzi, uonevu na hila na kukosekana
kwa demokrasia.
“Tumetoka CCM kwa sababu ya wizi wa
waziwazi katika uchaguzi, wanafunga magori ya mkono watu wakiwa wanaona, sasa
tumekuja huku upinzani. Lazima tuwashughulikea mpaka waachane na wizi wao.
“Niliwania udiwani kwa mara
nyingine tena, hila na tamaa ya CCM walinikata jina kwa sababu nilikuwa
napingana nao, walipolazimisha fedha za miradi ya wananchi tuzitumie kwa mambo
ya chama,” amesema Fashion.
Kwa upande wake, Jeremiah amesema
kutokana na CCM kushindwa kuwatumikia wananchi ipasavyo, sasa umefika wakati
wakaipisha UKAWA kuingia `magogoni` ili kutatua kero za watanzania.
HUKU ARUSHA NAPO MAMBO YALIKUWA HIVI
HUKU ARUSHA NAPO MAMBO YALIKUWA HIVI
Zaidi ya wanachama mia 300 waliokuwa chama cha CCM kutoka jamii ya kifugaji katika kata ya Engaruka wilaya ya Monduli wamezichoma kadi zao za CCM na kujiunga na CHADEMA huku wakidai maamuzi yao yametokana na utashi wao binafsi kwa kuzingatia hali halisi ya kisiasa ilivyo hivi sasa
Mamia ya wanachama walikusanyika katika mkutano wa hadhara kukusanya kadi za CCM kuzichoma moto na kuchukua kadi za CHADEMA.
Habari hii kwa hisania ya mwanahalis oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni