LOWASSA KUSIMAMISHA JIJI LA DAR KESHO,MJI KUFUNGWA,SOMA HAPO KUJUA
AGOSTI 10 mwaka huu, Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)
umekusudia kufanya msafara mkubwa wa kumsindikiza Edward Lowassa kuchukua fomu
ya kugombea urais katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi (NEC), Jijini Dar es Salaam. Anaandika Sarafina Lidwino …
(endelea).
Kwenye
msafara huo Lowassa ataongozana na mgombea mwenza wake Juma Duni Haji. Lowassa
alijiunga na Chadema Julai 28 mwaka huu akitokea Chama Chama Cha Mapinduzi
(CCM) huku Duni alijiunga Agosti 4 akitokea CUF.
Msafara huo utaanzia kwenye
Ofisi Kuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam saa 3:00 asubuhi ambapo wanachama wa
vyama vinavyounda umoja huo (Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF) watakutana na
kuanza safari ya kwenda NEC.
Baada ya Lowassa kuchukua fomu
NEC, msafara huo utaelekea Makao Makuu ya Chadema yaliyopo Mtaa wa Ufipa,
Kinondoni ambapo wateule hao watafanyiwa sherehe ya kupongezwa kwa hatua
waliyofikia.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema-Bara, Salim
Mwalimu akiwa kwenye Ofisi za NCCR-Mageuzi walipofanyia mkutano amesema,
wagombea hao wapo tayari.
Akifafanua kuhusu msafara huo
amesema, wagombea hao watasindikizwa na viongozi wa UKAWA, wanachama wa umoja
huo pamoja na wananchi watakaojitokeza kumsindikiza Lowassa.
Kuhusu suala la ugawanywaji wa
majimbo baina ya umoja huo Mwalim amesema “tumeshamaliza kila kitu na
tumeshagawana ila bado kutangaza tu muda ukifika tutawatangazia wananchi”.
Mbali na hilo Mwalimu
ameongelea kuhusu mbinu za wizi zinazofanywa na NEC kwa kushirikiana na Chama
tawala (CCM) ambapo amedai kuwa kumekuwa na malalamiko mengi toka kwa wananchi
ambao wanafanyiwa udanganyifu.
“Kumekuwa na wizi wa waziwazi
unaofanywa na CCM na tunasikitika kuwa tume ipo kimya ikionesha kuridhia na
matendo hayo. Vijijini watu wanaombwa namba zao za vitambulisho vya kura na
watu wanaodai wametumwa na serikali, sisi tumegundua tayari.
“Namba ya kitambulisho ni mali
ya mwananchi na sio ya serikali wala tume. Tumegundua mbinu zote zinazofanywa
na CCM ili waendelee kubaki madarakani ila wakae wakijua mawimbi haya hayawezi
kuzuilika kwani Ukawa ni chaguo la wananchi.”
Kuhusu kuachia ngazi kwa
aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba amesema, kuondoka kwake
hakuwezi kubomoa Ukawa wala kusambaratisha CUF.
"Ukawa bado tupo hai wala
hatutapoteza muda wetu kukaa kumlilia aliyejitoa kwani yawezekana mwezetu hana
ndoto ya matumaini ya kushika dola, anapenda tubaki chini,” amesema na
kuongeza;
“Nawapongeza sana CUF kwa
kuweza kulichukulia wepesi hilo na kutomjali kwa kujiuzulu kwake kwani
hakujaharibu chochote. Sisi bado tunasonga mbele na Jumatatu tutawasha moto
Ofisi Kuu ya CUF.”
Naye Tozzy Matwanga ambaye ni
Katibu Mkuu wa NLD amewataka wanachama wa chama hicho wote wajitokeze kwa wingi
siku hiyo katika msafara wa kwenda NEC.
“Pia tunaomba serikali
kuimarisha ulinzi pale unapohitajika. Hivyo hivyo kwa NEC wasimamie haki na
misingi ya kazi yao kwani damu ya wananchi ikimwagika wao ndio kitakuwa
chanzo.”
Hakuna maoni
Chapisha Maoni