HABARI KUBWA LEO,PINDA ASUSIA OFISI YAKE,ACHUKIZWA NA MCHAKATO WA URAIS CCM,SOMA HAPO KUJUA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodom picha na Maktaba |
WAZIRI mkuu
Mizengo Pinda amemsusia Ofisi Rais Jakaya Kikwete tangu kumalizika mchakato wa
kutafuta mgombea wa Urais ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM .(Mtandao huu
umedokezwa)Anaandika KAROLI VINSENT Endelea nayo.
Waziri mkuu Pinda ambaye alikuwa mtia
nia wa nafasi ya Urais ndani ya CCM na inatajwa kuwa jina lake lilikatwa katika hatua za mwanzo za
mchujo wa wagombe wa chama hicho.
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya
Ofisi ya Waziri mkuu zinasema kwa sasa Waziri mkuu Pinda ajarudi ofisini tangu
mchakato wa Urais wa CCM kumalizikia takribani mwezi mmoja sasa kwa kile
kinachoitwa ni “kutorizikia” na mchakato wa Urais ulivyoendesha ndani ya CCM ambao unatajwa ulikuwa ni uvunjifu wa kanuni za CCM.
Taarifa hiyo inasema kwa sasa
Pinda ameamua kususia Ofisi hadi masuala ya Siasa na kujichimbia Kijijini
kwake,akiendelea na shughuli mbali mbali ikiwemo kilimo.
Kwa mujibu wa Mtoa taarifa wetu aliyoko Kijijni kwa Pinda anasema waziri
mkuu huyo amechukizwa na rafu zilizofanyika wakati wa kuteua mgombea Urais
ndani ya CCM.
“Huyu bwana amekasirika sana na jinsi
alivyofanyiwa na Vigogo wa CCM,yaani kitu kinachomuumiza zaidi ni kwamba,Waziri
mkuu aliyekaa takribani miaka nane kwenye Utawala wa Kikwete,tena amemsadia
kwenye mambo mengi sana,leo aonekane hana maadili,kutokana na kitendo cha
Kamati ya Maadili kulikata jina lake,ndio anavyokuwa na Tafriri hiyo kwamba
yeye hana maadili anaumia sana”amesema.
Ameongeza kwa kusema kuwa “Pinda amepima miaka yote kwaanzia 1995,2005
mawaziri wa wakuu walikuwa wanapita hadi tano bora,anashangaa inakuwaje
yeye,yaani bora angechujwa kwenye kwenye kura za Nec,yaani anashangaa yote
aliofanyiwa,yaani anajiuliza wema wote aliomfanyia Kikwete kwenye utawala wake
ndio malipo anayolipwa ni fedheha hii”
Mbali na Waziri mkuu Pinda
waliochukizwa na hatua zilizotumika katika upatikanaji wa mgombea wa Urais wa
CCM ambaye amepatika Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli,mwengine ni Waziri mkuu wa
zamani Edward lowassa aliyejitokeza hadharani na kusema wazi wazi kwamba
mwenyekiti wa CCM,Jakaya kikwete alikuwa anawagombea wake mifukoni.
Viongozi wengine waliopinga mchakato
huo ni waziri Ofisi ya Rais asiyekuwa na wizara Maalum Profesa Mark Mwandosya
ambaye naye alimtupia Lawama Rais Kikwete pamoja na Kamati ya Maadili kuwa
waliokuwa na wagombea wao mifukoni.
Profesa Mwandosya ambaye ni Mbunge wa
Rungwe amesema hata vikao vya vya CCM vilikuwa vimepooza baada ya wanachama
kubaini michaakato ya kuteua mgombea Urais viligubikwa na ubabe.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni