KUMEKUCHA-VYAMA VYA UKAWA VYAONGEZEKA VYAFIKIA SITA,SOMA HAPO KUJUA
Wakati vyama vinne
vinavyounda UKAWA, vimempitisha Edward Lowassa kugombea urais, vyama vingine
vya SAU na APPT-Maendeleo vimetangaza kumuunga mkono mgombea huyo katika
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa SAU, Ali Kaniki alisema chama
hicho kimefikia uamuzi wa kuunga mkono umoja huo kutokana na nafasi kubwa
iliyopo ya kushika dola. Kaniki alisema kwa sasa wana wanachama zaidi ya
500,000 nchi nzima, hivyo wanaamini kuwa na mchango katika harakati hizo.
Mwenyekiti wa APPT-Maendeleo, Peter Mziray
alisema chama hicho kinaamini mabadiliko kupitia kambi ya upinzani, hivyo
wameamua kuunga mkono UKAWA.
“Uchaguzi wa mwaka 2010, nilishika nafasi ya
nne kwa kupata kura 96,000, lakini pia tuna madiwani watatu na wanachama
wameongezeka kwa hivyo ninaamini mchango wetu utakuwa na nafasi kubwa
UKAWA,”
Mwenyekiti wa UDP, Mkoa wa Dar es Salaam,
Joackim Mwakitinga alisema chama hicho kitakuwa tayari kuunga mkono mgombea
mmoja kutoka CCM au UKAWA.
“Nafasi ya urais hatutasimamisha mgombea ila tutaunga mkono kati
ya vyama hivyo wakati wa kampeni.”
Maoni 1
Patachimbika mwaka huu mpaka kieleweke tu
Chapisha Maoni