RAIS KIKWETE AWACHAFUA WASANII,USANII WAKE KWA WASANII WAPINGWA KILA KONA SOMA HAPO KUJUA
Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) akiwa katika hafla ya kuagwa na wasanii. Kushoto ni Katibu wa CCM, Abdulahaman Kinana. Kutoka kulia ni Waziri wa Sayansi na Tekinolojia, Januari Makamba na Mgombea wa CCM, John Magufuli. |
HAFLA inayotajwa
kuandaliwa na “Umoja wa Wasanii Tanzania” ya kumuaga Rais Jakaya Kikwete
anayestaafu baada ya uchaguzi wa Okotoba mwaka huu, imezua mjadala mkubwa
nchini.Anaandika Erasto Stanslaus … (endelea).
Mjadala wenyewe unatokana na kile ambacho
wengi wa wasanii wanasema kwamba hawajapata kujua kwamba kuna umoja wa wasanii
Tanzania.
Mingi ya mijadala inayoendelea kwenye
kota mbalimbali za jiiji la Dar es Salaam pamoja na mitandao ya kijamii
yanajadili kwamba kama ni umoja wa wasanii kumuaga Rais kikwete, imekuaje
ukumbi umejaa makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwepo mgombea Urais wa
chama hicho katika uchaguzi mkuu huo, John Magufuli.
Hoja kuu hapa ni, Je, umoja huo wa
wasanii umeundwa ndani ya mfumo wa CCM? au wasanii waliokuwa mbele katika hafla
hiyo walitumika tu kujenga picha kwamba umma wa wasanii Tanzania unamsapoti
Magufuli?
Ukweli ni kwamba, katika miongoni mwa
wasanii wenye majina makubwa katika tasnia ya filamu na muziki, ukiwemo wa
bongo fleva, taarabu, muziki wa injili na dansi, wapo wengi siyo tu ni viongozi
katika vyama vya upinzani, pia ni wagombea nafasi za ubunge kupitia vyama hivyo
vya upinzani.
Baadhi wa wasanii ambao ni wagombea ni
Seleman Msindi ‘Afande Sele’ na Joseph Haule ‘Prof. Jay’. Wasanii waliokuwa
meza kuu katika hafla hiyo sambamba na Kikwete ni Jacob Steven ‘JB’ na Nikii wa
Pili.
Yafuatavyo ni maswali
yanayouliwa katika mijadala iliyopo katika mitandao ya kijamii:-
1.
Umoja huo umeanzishwa
lini na viongozi wao kina nani?
2.
Wasanii wanatambua kua
kuna umoja wa wasanii tena usiokua na jina rasmi?
3.
Kama wasanii
wameungana ili kumuaga rais wa nchi, kwanini kulikuwa na lundo la viongozi wa
chama kimoja cha siasa?
4.
Magufuli kupewa nafasi
ya kipekee, alienda kama mgombea wa chama, kama waziri au kama mpiga ngoma
mtarajiwa wa Twanga?
5.
Nani aligharamia
gharama za sherehe?
6.
Wasanii walizipataje
hizo pesa za sherehe wakati wenzao wakiumwa hadi waandae matamasha ya kuchangia
kwa njia ya kiingilio na hawapati zaidi ya Sh. milioni mbili.
7.
Kwanini wasanii ambao
ndio wanaodaiwa kuwa waandaaji waliandaliwa kadi za mwaliko badala ya wao
kumuandalia mheshimiwa rais kadi ya mwaliko?
habari hii kwa hisani ya mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni